Habari za mikoani

Serikali- “Wahamasisheni Watoto Kusoma Masomo ya Sayansi”

Na.Thomas Lutego- H/W. Misungwi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amewaagiza Maafisa Elimu Sekondari kote Nchini kuwahamasisha wanafunzi wa Sekondari kupenda kusoma masomo ya Sayansi ili kuwa na taifa lenye wataalam wakutosha katika kipindi hiki cha mabadiliko ya Teknolojia na mahitaji ya sasa ya wataalam wa Afya ambapo hitaji limekuwa kubwa.

Habari za mikoani

Ireland Yawekeza zaidi ya shilingi Milioni 700 Kupambana na Ukatili Wilayani Misungwi

SERIKALI ya Jamhuri ya Ireland kupitia Shirika la Maendeleo nchini humo limetoa msaada wa kiasi cha Uero 350,000 (zaidi ya milioni 700) kwa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwezesha mpango wa kujenga uwezo wa jamii na taasisi za Serikali ili kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata 10 wilayani Misungwi mkoani hapa.