Afya

TANGAZO LA UFADHILI-MARUDIO

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anawatangazia wanafunzi wote walioko vyuoni na wale wote waliopata udahili wa masomo ya Uzamili katika fani za Afya kwa mwaka wa masomo 2017/2018, kuwa muda wa kuwasilisha maombi umeongezwa hadi tarehe 19/01/2018. Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada pamoja na posho ya utafiti pindi mwanafunzi anapokuwa kwenye kipindi cha kufanya utafiti kama sehemu ya mafunzo yake. Kwa wanafunzi waliokwisha wasilisha maombi yao, hawatakiwi kuomba upya.
Vigezo vilivyowekwa […]

Habari za mikoani

RC Shinyanga Awashukia Viongozi na Kuwatimua

Mkuu wa Mkoa Mhe. Zainab Telack akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiangalia uharibifu uliofanywa kwenye vyumba vya madarasa vinavyojengwa baada ya kuchimbwa ili kutafuta madini ya almasi kulikofanywa na wajumbe wa kamati ya shule ya msingi jitegemee kwa kushirikiana na Serikali ya kijiji cha Maganzo Wilayani Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameivunja Serikali ya kijiji cha Maganzo […]

Habari za mikoani

Mtwara-Mikindani Yatumia zaidi ya Mil. 830 Kutekeleza Miradi ya Maendeleo.

Ujenzi wa Shedi ya Mwalo wa Mikindani, Huu ni Mmoja ya Miradi iliyotekelezwa kwa Fedha hizo.
NaJamadi Omari- H/Manispaa Mikindani

Katika kuhakikisha kuwa Manispaa Mtwara-Mikindani inaendelea kuboresha huduma za Jamii kwa Wananchi wake, imetoa na kutumia fedha kiasi cha shilingi milioni  834,074,361.79 kutoka katika mapato yake ya ndani Kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwepo  kuchangia mfuko wa Wanawake na Vijana pamoja na ulipaji fidia kwa […]

Habari za mikoani

Bolisa Walilia Mitaro kwa TARURA

Hali ya Mitaro katika Barabara ya Bolisa Halmshauri ya Mji Kondoa.
Na. Sekela Mwasubila
Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kutengeneza mifereji pembezoni mwa barabara zilizofanyiwa matengenezo ili kuwa na barabara zinazopitika muda wote.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Bolisa Mh. Abed Boki alipokuwa akiongelea juu ya hali ya barabara ya kuelekea Bolisa kutoka Kondoa Mjini kwa […]