Month: April 2018
Simiyu kupata Shule ya Vipaji Maalum, Kuchagiza Viwanda Mkoani humo
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Malambo Mjini Bariadi wakichimba msingi wa wa ujenzi wa madarasa zaidi 40 na mabweni 15 ya Shule ya Sekondari Simiyu ambayo inatarajiwa kuwa shule ya vipaji maalum ya mkoa wa Simiyu.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wananchi wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga wamejitokeza kwa wingi kuchangia nguvu kazi , […]
Magzetini Leo
Serikali: Madarasa ya Awali kwa kila Shule ya Msingi ifikapo 2020
Naibu Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda akitoa ufafanuzi wa zaidi kuhusu Elimu ya Awali katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kwenye kipindi cha Haba na Haba
Naibu Waziri Ofisi ya Raisi (TAMISEMI), Joseph Kakunda, alisema serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha kila shule ya Msingi inakua na darasa […]
Zoezi la Kubaini Watoto wenye Mahitaji Maalum nchini Lafanikiwa
Na. Fred Kibano- TAMISEMI
Zoezi la kuwabaini watoto wenye mahitaji maalum chini ya Mpango wa kukuza stadi za kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) linaloendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambalo lilianza wiki tatu zilizopita ni la mafanikio makubwa.
Akiongea mjini Morogoro wakati wa kikao na timu ya kubaini watoto hao kwa mkoa wa Morogoro, Mratibu wa Mpango huo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Julius Migea amesema zoezi hilo limeisaidia Serikali kupata takwimu na mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum na hivyo […]
Manispaa ya Iringa yatoa Mikopo kwa Wanawake na Vijana
mkopo vijana
Baraza la Madiwani Mbulu laipongeza Serikali
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mbulu limeipongeza serikali kwa kusimamia maamuzi ya ujenzi wa Makao Makuu kuwa Dongobesh kutokana na mapendekezo ya baraza na hata baada ya ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Manyara iliyofanyika tarehe 04-09/03/2018 ambapo alishauri kuwa ujenzi ufanyike Haydom na kuwaagiza Mwenyekiti na Mkurugenzi kuitisha baraza maalum ili kujadili maoni hayo.
Waheshimiwa […]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli awaongoza watanzania katika sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Jijini Dodoma
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.Aprili 26,2018.
Continue Reading
Dodoma sasa Jiji rasmi
Na. Atley Kuni – OR-TAMISEMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameupandisha hadhi Mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji, na amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo tarehe 26 Aprili, 2018 wakati akihutubia katika sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Pamoja na […]