Habari za Wizara

Jafo Atoa Wito Kusaidia Wanafunzi Wasiojiweza ili Kuinua Elimu

Na. Zulfa Mfinanga
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo, leo amekabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza wa shule ya msingi na sekondari za Kata ya Sejeli kijijini Mbande wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Msaada huo utanufaisha zaidi ya wanafunzi mia tisa ni pamoja na madaftari 9,000, kalamu 4,000, penseli 2,800, vifutio 1,200 na vichongeo 1,200 vyote vikiwa ni msaada kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Makao makuu […]