Elimu

Serikali yagawa Pikipiki 2894 kwa Waratibu Elimu Kata nchini

Na Mathew Kwembe Dar es salaam
Serikali imezindua zoezi la usambazaji wa pikipiki 2,894 kwa Waratibu Elimu kata nchini kwa kutoa wito kwa Maafisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha kuwa pikipiki hizo zinawafikia walengwa hao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa funguo za pikipiki hizo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amewataka Maafisa wa Elimu kuhakikisha kuwa pikipiki hizo aina […]