Mafunzo

Kakunda Awataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya Wapya kuacha Mivutano

Na. Magdalena Dyauli na Fred Kibano
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia ELIMU Joseph Kakunda amefungua rasmi mafunzo kwa Wakurugenzi wapya wa Halmashauri na Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli hivi karibuni Jijini Dodoma leo.
Kakunda amewataka Viongozi hao kutambua kuwa wao ni tegemeo kubwa katika utekelezaji wa Sera za Serikali hivyo ni muhimu kujua wajibu wao, hasa kwa kuhimiza ushirikiano kwenye utekelezaji wa […]