Habari za mikoani

Ubalozi wa Japan Kujenga Sekondari Keikei Kondoa

 
Na. Sekella Mwasubila- H/Mji Kondoa
Ubalozi wa Japan umeahidi kujenga Shule ya Sekondari ya kata ya Keikei ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya kata ya Busi inayohudumia wanafunzi wa kata mbili.
Ahadi hiyo ilitolewa na mwakilishi wa ubalozi wa Japan Bwana Takao Kurukawa katika kata ya Keikei alipofika katika eneo lililotengwa  kwaajili ya ujenzi wa sekondari hiyo hivi karibuni.
“Nimekuja kuangalia eneo ambalo litajengwa Shule ya  Sekondari na ubalozi wa Japan baada ya kupokea maombi ya kuomba kujengewa shule […]