Elimu

Waziri Jafo: Shule ya Sekondari Bihawana kufanyiwa Ukarabati Mkubwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akikagua Maktaba ya Shule ya Sekondari Bihawana wakati alipotembelea shule hiyo kukagua miundombinu ya shule kabla ya kuanza Ukarabati Mkubwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akasikitishwa na uchakavu wa miundombinu ya Jiko la Nje katika shule ya Sekondari Bihawana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiendelea na Ukaguzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Bihawana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akisafisha mikono yake Sink la shule ya Sekondari Bihawana.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Bihawana.

Angela Msimbira- OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema serikali imeamua kukarabati shule ya Sekondari ya Bihawana ili kuweka mazingira bora ya mwanafunzi kujifunzia.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika shule hiyo iliyopo katika Manispaa ya Dodoma na kukagua miundombinu  ya shule ya Sekondari ya Bihawana kabla ya ukarabati mkubwa  unaotarajia kuanza  hivi karibuni.

Akielezea lengo la ziara Waziri Jafo amesema  ni kukagua  uchakavu wa majengo wanayotumia wanafunzi na kupata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mshauri kile wanachotarajia  kufanya baada ya kufanya tathmini ya kina kinachohitajika  katika kazi ya ukarabati wa shule hiyo.

Waziri Jafo amesema baada ya kufanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya shule amegundua kuwa kunauchakavu mkubwa wa mabweni, ofisi ya waalimu, madarasa, bwalo, jiko lakini nimegundua uchakavu  mkubwa upo kwenye vyoo na ukosefu wa maji katika shule hiyo.

Waziri Jafo amesema serikali imepanga kuibadilisha shule ya Sekondari ya Bihawana na kuwa ya kisasa na kuwa kivutio kwa wazazi kuwaleta watoto wao katika shule za Sekondari,na kuwafanya wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga hapo kujiskia fahari kupata Elimu yao katika mazingira bora na rafiki kwa kujifunzia.

“Ninataka kuibadilisha shule ya Sekondari ya Bihawana kuwa shule yenye Kuvutia  kiasi ambacho Walimu watafanya kazi katika mazingira bora, watumishi wa hapa na wanafunzi pia na zaidi wale wanafunzi waliomoa hapa miaka ya nyuma wakija shuleni hapa wapotee kwa kukuta mazingira tofauti nay ale waliyo yaacha”amesema Jafo.

Shule hii iko katika mpango wa Serikali wa Uboreshaji miundombinu ya Shule ya kongwe  89 na Shule hii inaanza kukarabatiwa katika awamu ya pili ya mpango huu na Ukarabati huo utagharimu zaidi ya Tsh Mil 500.

 

 

 

CAPTION:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *