Habari Kitaifa

Chamwino Waagizwa Kukamilisha Jengo la Halmashauri

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

Na Mwandishi wetu TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameiagiza Wakala wa Majengo (TBA) na Suma JKT kuangalia njia bora ya kukamilisha ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino haraka na kwa ubora unaotakiwa.

Amesema hayo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo hii leo.

“TBA na Suma JKT fanyeni tathmini ya jengo hili na muweke mkakati wa kulikamilisha haraka iwezekanavyo ili watumishi wahamie katika jengo hilo” amesema Mhe. Jafo

Mhe. Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na kwamba kwa kuwa wanaelekea katika mipango ya bajeti wataangalia namna ya kushirikiana na Halmashauri ili jengo liweze kukamilika.

Pamoja na Changamoto zilizoainishwa na Wakandarasi haoMhe. Jafo ameongeza kuwa jengo hilo ni lazima likamilike ili watumishi wa Halmashauri hiyo wahamie ili kuboresha utendaji kazi wao.

Amesema

“kutokana na sababu zilizotolewa na mkandarasi ni vyema watumishi wakaendelea kuvumilia kutumia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hadi hapo itakapokamilika kwenye ubora unaotakiwa

 Akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari mosi mwaka huu Mhe. Jafo amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa  kukwama kukamilishwa kwa jengo hilo.

amesema wanafanya tathmini katika jengo hilo kuangalia namna ya kulikamilisha kwa kushirikiana na. Aidha Mkandarasi Mshauri kutoka TBA, Mhandisi Vilumba Sanga

Awali, Mkandarasi kutoka Suma JKT, Mhandisi David Pallangyo amesema ukamilishaji umekwamishwa kutokana na hali ya hewa na pia makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali.

“Hapa hii flow ya chini tuliona tuikamilishe lakini hali ya hewa na hizi mvua maji yanajaa hivyo tunafanya tathmini kama tutaweza ni vyema tukaweka water proof,”amesema

 “Tunafanya ‘estimate’ ya water proof maana maji yanajaa, hii inatokana na makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali, huyu mkandarasi wa sasa anakutana nayo site,”amesema Sanga

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ametembelea Kituo Cha Afya cha Chamwino Ikulu kuangalia uboreshaji wa kituo hicho ambacho kimeingiziwa Sh.Milioni 500 kwa ajili ya kujenga Wodi ya akina mama na watoto, maabara, Chumba cha Kuhifadhia maiti.

Hata hivyo, amekuta ujenzi huo haujaanza kutokana na eneo linalotakiwa kujengwa kuwa dogo na hivyo kuahidi kufanya tathmini halisi kwa kushirikiana na wataalam kuangalia uwezekano wa kujengwa jengo la ghorofa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kujionea eneo litakalotumika kuongeza majengo ya Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamonga wakati akitoa maelezo kuhusu eneo lililotengwa kwa ajili ya uboreshaji Kituo cha Afya Chamwino.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *