Habari za Wizara

Ajira Mpya TEHAMA Wapigwa Msasa

Na. Nteghenjwa Hosseah-OR TAMISEMI, Dodoma

Watumishi wapya wapatao 70 wa kada ya TEHAMA walioajiriwa Mwezi Februari, 2019 na kupangiwa OR-TAMISEMI Makao Makuu, Sekretariet za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) wanaendelea kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu mifumo ya TEHAMA inayosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma. Shabaha ikiwa ni kuwafanya kuijua mifumo iliyopo lakini pia kuihudumia mifumo hiyo.

Akizungumza wakati wa mafunzo Msimamizi wa mafunzo hayo Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, James Mtatifikolo, amesema mafunzo hayo ya siku tano yatakuwa na faida kwao kwani kila uchwao teknolojia inakuwa na hivyo kuwajengea uwezo wasimamizi wa mifumo ni suala muhimu kwa sasa.

“OR-TAMISEMI ina mifumo zaidi ya ishirini ambayo inatumika moja kwa moja kwenye ngazi za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na taaisisi zake, ambayo  mingi  inatumika mpaka kwenye vituo vya kutolea huduma kama Shule na Vituo vya kutolea huduma za Afya, hivyo tumeona ni vyema wataalam wetu hawa wapya wakapatiwa mafunzo ili wapate uelewa mzuri wa namna bora ya kuisimamia mifumo hiyo” AlisemaMtatifikolo.

Mmoja ya  wakufunzi wa Kitaifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Stephano Amoni amesema kuwa, Maafisa TEHAMA wanaoendelea na mafunzo wako vizuri na wanashiriki kikamilifu katika mafunzo husika jambo ambalo linafanya kazi ya ukufunzi kuwanyepesi.

“Unajua unapofundisha watu ambao wanajua nini wanakifanya  katika mifumo na wanaelewa vizuri mambo ya TEHAMA kazi inakuwa nyepesi kinacho bakia ni kuwapa mambo ya msingi tu, ambayo wataenda kukutana nayo katika mifumo hii ambayo ndio kwanza wanakutana nayo kwa mara ya kwanza.”alisema Amoni.

Kwa upande wake, Afisa Tehama kutoka Halmashari ya Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora Ludao William anasema, mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuwaongezea ujuzi na uelewa wa kushughulikia mifumo mingi zaidi.

“Unajua sisi kila mmoja wetu ana uelewa wa mifumo sema tu hii ya OR-TAMISEMI hatuwajahi kuifanyia kazi hivyo Elimu tunayoipata hapa itatufanya tuwe Maafisa TEHAMA bora zaidi katika Halmashauri na Mikoa”

Mafunzo haya ya siku tano yanafanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga na yanaendeshwa na Wataalam toka OR-TAMISEMI, Wakufunzi wa Kitaifa kutoka kwenye Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *