Habari za Kijamii

Mgogoro wa Kyoruba na Kebwehe wamalizika Wilayani Tarime

Na Fred Kibano
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akiwasihi wananchi wa vijiji vya Kyoruba na Kebwehe wilayani Tarime kuacha mapigano na kuendelea kuishi kwa amani na utulivu. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Charles Kabeho
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amewasihi wananchi wa vijiji vya Kyoruba na Kebwehe kuacha mapigano kama […]

Habari Kitaifa

Nyamhanga aagiza Kukamilika barabara ya sabasaba – Buswelu mkoani Mwanza

Na Fred Kibano
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amepongeza ujenzi unaoendelea wa barabara ya sabasaba kupitia Kiseke hadi Buswelu yenye urefu wa kilomita 9.7 na kumtaka mkandarasi SINO Hydro Ltd wa China kumaliza kazi kwa wakati.
Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 9.7 ina umuhimu mkubwa itafungua kwa kiasi kikubwa Manispaa ya Ilemela, Manispaa ya Nyamagana na Jiji la Mwanza na kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi.
Aidha, Nyamhanga amesema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI […]

Elimu

Serikali Yaagiza Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya Kusimamia Taaluma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi Isenga D (hawapo pichani) iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza  na kutoa maagizo ya Serikali alipofanya ziara shuleni hapo  jana. Kushoto kwake ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Warioba Sanya na Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Michael Ligola