Habari za Wizara

Halmashauri zaagizwa kuitumia vizuri mifumo ya kielektroniki

Na Mathew Kwembe, Kagera
Watendaji wa Halmashauri nchini wameagizwa kuitumia vizuri mifumo mbalimbali ya kielektroniki iliyowekwa na Serikali kwa kushirikiana na Mradi wa PS3 katika halmashauri zote 185 nchini ili mifumo hiyo iweze kufanya kazi yake kwa malengo yaliyokusudiwa.
Agizo hilo limetolewa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Kamishna wa Polisi Diwani Athuman wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya Mfumo wa Epicor toleo la 10.2 kwa Waweka hazina, Wahasibu na Maafisa Wasimamizi wa Fedha kutoka Mikoa ya Mara na […]

Elimu

UMISSETA kufanyika Dodoma mwakani

Na Mathew Kwembe, Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ametangaza kuwa mashindano ya michezo ya Umoja wa Michezo wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yatafanyika mkoani Dodoma.
Kwa miaka mitatu mfululizo mashindano hayo yamekuwa yakifanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya chuo cha ualimu Butimba.
Akifungua rasmi mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kwa mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba jana Waziri Mkuu alisema kuwa pamoja na mkoa wa […]

Elimu

Mashindano ya UMISSETA yaendelea jijini Mwanza

Na Mathew Kwembe, Mwanza
Mashindano ya UMISSETA yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba na Shule ya Sekondari Nsumba yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa mnamo tarehe 9 juni 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hadi kufikia jana mashindano hayo yameshuhudia michezo mbalimbali ikichezwa katika viwanja vya Nsumba na Butimba ambapo jumla ya mikoa 28 inashiriki mashindano hayo
 
Continue Reading

Elimu

Mikoa ya Iringa na Kagera yatamba fainali riadha maalum

Na Mathew Kwembe, Mwanza
Washiriki wa mchezo wa riadha maalum kwa mbio fupi kutoka mikoa ya Iringa na Kagera wametamba katika mashindano ya UMISSETA yaliyofanyika jana katika viwanja vya Butimba baada ya kushika nafasi tatu za juu kutoka mikoa hiyo.
Katika mchezo wa riadha maalum hatua ya fainali kwa mbio fupi za mita 100, washiriki wawili kutoka mkoani Iringa ambao ni Mathias Peter aliyetumia sekunde 12: 72 na Sudy Bakari aliyetumia sekunde 13:20 ambao kwa pamoja waliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya […]

Habari za Wizara

Mfumo wa uhasibu kuongeza uwazi na uwajibikaji katika halmashauri


Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Baltazar Kibola, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Epicor toleo la 10.2 kwa Wahasibu na WawekaHazina kutoka Mikoa ya Morogoro, Iringa  na Halmashauri za Jiji la Tanga, Muheza na Korogwe
Serikali imesema kuwa maboresho iliyoyafanya kwa kushirikiana na Mradi wa PS3 ya kuwa na mfumo mmoja […]

Elimu

Jafo apiga marufuku mamluki kushiriki UMISSETA na UMITASHUMTA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa mashindano ya UMISSETA iliyoanza leo katika viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba kilichopo jijini Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa mikoa […]