Habari za Wizara

Serikali yafanya Mapitio ya Sera ya Ugatuzi wa Madaraka


Zulfa Mfinanga
SERIKALI imeanza kufanya uchambuzi wa kina juu ya kazi mbalimbali za serikali zinazofanyika katika dhana ya ugatuzi wa madaraka kwa lengo la kuboresha sera mpya ya ugatuzi wa madaraka ili iwe kwenye mfumo wa kisheria.
Hayo yamezungumzwa leo na Naibu Katibu Mkuu elimu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Tixon Nzunda kwenye warsha ya mapitio ya sera ya ugatuaji wa […]

Habari za mikoani

Mil. 400 Kuboresha Miundombinu Kituo Cha Afya Uyovu, Bukombe

Tusa Daniel, Bukombe
Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imepokea jumla ya Tsh.400,000,000/= kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia udhamini wa Benki ya Dunia kwa ajili ya maboresho ya Kituo cha Afya Uyovu ili kiweze kutoa huduma ya upasuaji wa dharura kwa kinamama wajawazito. Hii ikiwa ni awamu ya pili ya mpango wa Serikali wa maboresho ya vituo vya kutolea huduma za Afya.
Fedha hizi zimelenga kujenga Wodi ya Wazazi (Maternity ward) 1, Wodi ya Watoto (Paediatric […]