Afya

Bahi wapongezwa, Ujenzi wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya

Nteghenjwa Hosseah, BAHI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda wakati wa zaiara yake ya kukagua ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Bahi

  1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Bahi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Bahi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiangalia matofali ambayo yanafyatuliwa na mgambo ambao wamepewa kazi hiyo kwa ajili ya kurahisisha kazi ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya

Muonekano wa moja ya jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya Hospital ya Wilaya ya Bahi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya unaoendelea katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza kati ziara yake ya kikazi wilayani humo Jafo ameonyesha kuridhishwa kwake na wakati anapokea Taarifa ya Wilaya hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Afya na kisha kutembelea ujenzi wa Hospital ya Wilaya ambayo ipo katika hatua ya lenta.
“Hakika Bahi mmefanya kazi nzuri mmejenga kwa kasi ya ajabu huku ubora ukizangatiwa katika majengo yote na bado mmesimamia matumizi mazuri ya fedha za mradi kwa kuwapa vibarua kazi hii ya ujenzi.
Niseme wazi kuwa Bahi mmenifurahisha kwa sababu mmeweza kutafsiri vizuri mfumo wa ujenzi pasipo kutumia MKandarasi yaani “Force Account” ambao unatumia fedha kidogo na mmeweza kutumia nguvu kazi mliyonayo ya mgambo kufyatua matofali na vibarua ambao ni vijana kutoka hapa hapa Bahi kujenga majengo ya Afya hongereni sana kwa hili” Alisema Jafo.
Sambamba na kuwapongeza viongozi hao pia aliwataka kumaliza tofauti zilizopo kati ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na Mbunge kwa kuwasisitiza kila mmojawao kutekeleza majukumu yake pasipo kuingiliana wala kukwamishana.
“Lengo letu sote ni kuleta maendeleo kwa Wananchi kwahiyo Mwenyekiti wa Halmashauri tekeleza majukumu yako pasipo kumuingilia Mbunge na Mbunge naye aendelee kutekeleza majukumu yake ya Kibunge tena anafanya vizuri sana na miradi yote hii mnayopata ni jitihada zake Bungeni kwahiyo msimkwamishe mpeni ushirikiano wa kutosha” Alisema Jafo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belinith Mahenge amemueleza Waziri Jafo kuwa Wilaya ya Bahi ni moja kati ya Wilaya za Dodoma zinazofanya vizuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa ujenzi wa vituo vitatu vya Afya umeshakamilika na vitafunguliwa hivi karibuni wakati hospotali ya Wilaya ikiwa katika hatua ya lenta.
“Pamoja na changamoto chache ambazo tunakutana nazo katika utekelezaji wa miradi hii kama vile ushiriki mdogo wa wananchi katika kuchangia nguvu kazi, kukosekana kwa Mhandishi wa Halmashauri lakini tumeweza kukabiliana nazo na kuhakikisha hazikwamishi ujenzi wa miradi yetu ya Afya” Alisema Munkunda.
Ujenzi wa Hospital za Wilaya unaondelea kote Nchini unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *