Habari za mikoani

Baraza la Madiwani Mbulu laipongeza Serikali

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mbulu limeipongeza serikali kwa kusimamia maamuzi ya ujenzi wa Makao Makuu kuwa Dongobesh kutokana na mapendekezo ya baraza na hata baada ya ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Manyara iliyofanyika tarehe 04-09/03/2018 ambapo alishauri kuwa ujenzi ufanyike Haydom na kuwaagiza Mwenyekiti na Mkurugenzi kuitisha baraza maalum ili kujadili maoni hayo.

 Waheshimiwa Madiwani wakiwa ukumbini kuendelea na mjadala wa kikao

Akiongea kwenye kikao hicho kilichofanyika hii leo tarehe 25/04/2018, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph Mandoo amewaomba Waheshimiwa madiwani kutumia kikao hicho kuweza kupanga na kusimamia maendeleo ya Halmashauri kwa ujumla.

“Napenda kutumia fursa hii kuipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Joseph Magufuli na Uongozi wake kwa ujumla kwa kuwa makini na kusimamia kile kinachotekelezwa kwa umakini na  Watendaji wake wa chini wanachokipanga na kukipitisha ili kuleta maendeleo kwa wananchi”, amesema Mhe. Mandoo kwenye kikao cha baraza hilo.

 Mhe. Joseph G. Mandoo Mwenyekiti wa Halmashauri  akisoma kwa makini muhtasari unaowasilishwa

Kufutia vikao vya Kisheria vilivyokaa kwa ngazi tofauti vya maamuzi, uongozi ulipokea rasmi barua ilikielekeza ujenzi huo ufanyike katika Mji wa Dongobesh kama ilivyokuwa mapendekezo ya Baraza la Waheshimiwa Madiwani. Mhe. Mandoo ametoa ufafanuzi wa kina kuwa taratibu zote za kisheria zimezingatiwa na taratibu za kuthamini mali na ardhi pia zimefuatwa na hivyo kuomba taratibu za ujenzi kuanza mara moja katika eneo husika.

 Kaimu Mkurugenzi Ndugu Michael Faraay akipitia baadhi ya nyaraka zinazowasilishwa na kamati mbalimbali

Akitoa maagizo ya Serikali juu ya ujenzi huu wa makao makuu, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Chelistino Mofuga ameshauri baraza la Madiwani kupitia Mwanasheria wa Halmashauri waweze kuzingatia taratibu zote za kimikataba kwa wananchi waliotoa ardhi yao ipatayo hekta 102.

Mhe. Chelestino Mofuga Mkuu wa Wilaya ya Mbulu akiwa katika kikao cha baraza

Aidha Mhe. Mofuga ametumia fursa hiyo kukemea vikali taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao kuhusu maandamano na kuliagiza jeshi la Polisi kuanza doria mara moja, na kutoa onyo kali kwa watumishi watakaobainika kujihusisha na kuhamasisha maandamano hayo hatua kali zitachukuliwa juu yao.

baadhi ya Wataalam waliohudhuria kikao, kutoka kulia ni Afisa Mipango, Mweka hazina na Afisa Utumishi

Akihitimisha kikao hicho cha baraza, Mwenyekiti wa halmashauri awaomba wataalam kusimamia na kutekeleza ipasavyo maagizo waliyotoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *