Habari za Wizara

Bil 2.8 Zatumika Kutatua Changamoto Za TARURA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 26 ya Wakala wa barabara za mjini na vijijini(TARURA),kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seif.

Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seif akitoa taarifa ya utangulizi na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi magari 26 ya Wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 26 yaliyonunuliwa na Serikali na kuyakabidhi TARURA tayari kwa matumizi katika Halmashauri mbalimbali Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Ndani ya Gari) akiendessha Gari baada ya uzinduzi wa magari 26 ya TARURA.

Katika Picha ya Pamoja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Katikati)pamoja na Menejiment ya TARURA.

Baadhi ya magari yaliyokabidhiwa kwa TARURA.

 

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Kutokana na uchanga wa Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) ambapo ina mwaka sasa tangu kuanzishwa kwake bado inakabiliwa changamoto ya uhaba wa vitendea kazi, majengo ya Ofisi katika ngazi ya Halmashauri na Mikoa pamoja na ufinyu wa bajeti ikilinganishwa na mahitaji.

Katika kukabiliana na changamoto hizo  eneo la uhaba wa vitendea kazi ambalo ni pamoja na  magari ya usimamizi wa kazi mbalimbali zinazotekelezwa na TARURA, Serikali kwa kuliona hilo imeona ni vyema kutatua changamoto katika maeneo mbalimbali yenye Uhitaji hususani uhaba wa vitendea kazi kama magari ya usimamizi wa shughuli za barabara.

Llengo ni  kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na hatimaye kuchochea kazi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Katika Mwaka wa Fedha 2017/18 Serikali imetumia zaidi ya Tsh Bil. 2.8 katika ununuzi wa magari 26 ambayo yamekabidhiwa kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) na kufanya Wakala kuwa na idadi ya magari 288 kati ya Magari 440 yanayohitajika.

Akikabidhi magari hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema magari haya yanayokabihdiwa leo yakasaidie katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Barabara ili kuhakikisha kuwa kila shilingi inayotolewa na Serikali inatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Natoa Rai kwa TARURA mhakikishe mnayatunza magari haya ili yakafanikishe malengo ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa ufanisi, na madereva wote watakaokabihidwa wapewe maelekezo ya kuwa makini katika kuyahudumia ipasavyo kila inapotakiwa ili yaweze kuduma kwa muda mrefu” alisema Jafo.

Pia aliwakumbusha wataalamu wote wa TARURA kufanya kazi kwa Weledi ili kuleta matokea ya haraka katika sekta ya barabara ambayo inategemewa sana na imekua chachu katika kukuza uchumi wa Taifa letu.

Naye Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seif ameishukuru Serikali kwa kuwapatia magari ambayo tataongeza ufanisi katika utendaji kazi wa TARURA pia alibainisha kuwa katika Bajeti ya mwaka wa Fedha 2018/19 Serikali imetenga Tsh. Bil 2 kwa ajili ya kununua magari mengine 20.

Serikali ilianzisha Wakala wa Babarabara za vijijini na mjini (TARURA) kwa sharia ya Wakala wa  Serikali Sura ya 245 na kutangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Na. 211 la tarehe 12/05/2017 na kuzinduliwa rasmi mnamo mwezi Julai,2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Majaliwa(MB).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *