Habari katika Picha

Boresheni Utendaji wenu Tufikie Uchumi wa Viwanda

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda, amezungumza na watumishi wa halmashauri za Mji na Wilaya Tarime alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime na kuwataka kuimarisha utendaji wao wa kazi ili kuboresha zaidi huduma za jamii Serikalini.
Nzunda pia amezungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi ili kufikia malengo tarajiwa ya Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa sekta ya elimu na uwajibikaji kazini kwa watumishi wa Umma kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati viwanda.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri za Mji na Wilaya Tarime wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda alipofanya ziara wilayani Tarime

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *