Elimu

Serikali Kuboresha Elimu ya Watoto wenye mahitaji maalum

Na Fred J. Kibano
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Tixon  Nzunda amefungua mafunzo kwa walimu wa shule zenye  wanafunzi wenye mahitaji maalumu  , Maofisa wa Ustawi wa Jamii na  Maofisa Elimu Maalum ngazi za wilaya na Mikoa yote ya Tanzania Bara.
Akifungua mafunzo hayo ya siku sita mjini Morogoro, Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) TAMISEMI, Tixon  Nzunda, amesema  Ofisi ya Rais TAMISEMI imepanga kufanya  zoezi  maalumu la kuwatambua watoto wenye ulemavu wa aina tofauti  ili  watabuliwe  kwa ajili ya kupata afua sahihi na mahitaji maalumu  ya kielimu  mashuleni.
Amesema mafunzo   hayo maalum  yamelenga kuwapatia mbinu mbalimbali […]

Elimu

Kakunda Apongeza Taasisi Zilizoteleleza Mradi Wa Fursa Kwa Watoto

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Kakunda amezipongeza Taasisi za Children in Crossfire pamoja na TAHEA kwa utekelezaji mzuri wa mradi wa fursa kwa watoto.
Mhe. Kakunda ameyasema hayo wakati akifunga mradi wa fursa kwa watoto unaotekelezwa na kuratibiwa na Taasisi ya Children in Crossfire kwa kushirikiana na TAHEA katika Mkoa wa Mwanza na Maarifa ni ufunguo katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Continue Reading

Elimu

Waziri Jafo awataka Wadau wa Elimu kuunga mkono Sera ya Elimu Bila Malipo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo (Mb), akitoa msaada uliotoka kwa Wadau wa Elimu wa karatasi maalum kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wasioona kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri Wasioona wakati wa uzinduzi wa Kampeni ambayo Mhe. Jafo ameiita “NISAIDIE DAFTARI NA PENI NAMI NIPATE ELIMU” tukio hilo […]

Elimu

Walimu Mbarali Waaswa kuwa Kielelezo cha Tabia Njema.

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Taifa Oliver Mhaiki wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya
Na Daudi Nyingo- H/W Mbarali
Walimu kote nchini wametakiwa kuwa kioo na kielelezo muhimu cha maadili kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Taifa Oliver Mhaiki wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya kwa […]