Habari Kitaifa

Kakunda anusa harufu ya Ufisadi Halmashauri ya Ulanga Morogoro

Na. Fred Kibano       
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe. George Kakunda, ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina kwa miradi ya maendeleo baada ya kubaini ubadhilifu wa mamilioni ya shingi katika halmashauri ya Ulanga.
Mhe. Kakunda ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika halmashauri hiyo ambapo amemwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe, kuunda timu maalum kufanya uchunguzi kwa miradi ya maendeleo pamoja na fedha za Serikali.
“lazima timu ichunguze hilo greda kama […]

Habari Kitaifa

Rais Magufuli Awajibu Wanaokosoa Mpango wa Walimu wa Sekondari kupelekwa Shule za Msingi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewajibu watanzania ambao wanakosoa mpango wa serikali wa kuwapeleka walimu wa sekondari kufundisha shule ya msingi.
Rais Magufuli amesema kuwa kitendo hicho ni cha kawaida kwani hakiadhiri mishahara yao bali kinawapa muda mwingi walimu hao kufanya kazi nyingine za ziada.
“Wakati wa Nyerere walikuwa wanachukuliwa walimu […]

Habari Kitaifa

Dodoma sasa Jiji rasmi

Na. Atley Kuni – OR-TAMISEMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameupandisha hadhi Mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji, na amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi  kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo tarehe 26 Aprili, 2018 wakati akihutubia katika sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Pamoja na […]

Habari Kitaifa

Hati Safi Zaongezeka Katika Mamalaka za Serikali za Mitaa

 

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Bunge, mapema leo ktolea ufafanuzi hoja zilizobainishwa kwenye Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
 
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, […]

Habari Kitaifa

Waziri Jafo Atoa Maagizo Mazito kwa Viongozi wa Mikoa na Halmashauri

Lilian, Lundo – Maelezo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Selemani Jafo akisisitiza umuhimu wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kutimiza wajibu wao kwa kuisemea Serikali katika maeneo yao kwa kuzingatia weledi na kujituma wakati akifunga Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini mapema leo jijini Arusha.
Continue Reading

Habari Kitaifa

Mapinduzi Makubwa Bajeti za Halmashauri 2018/19

Wataalam wachambuzi wa Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakiwa katika zoezi la uchambuzi wa bajeti za mamlaka hizo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, ni Bajeti ya 2018/19 ambapo bajeti hizo zimefanywa kwa mfumo mpya wa PlanRep iliyoboreshwa.
Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI
Timu ya wataalam 50 kutoka Makao Makuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri imefanikiwa kukamilisha […]

Habari Kitaifa

Waziri Jafo, ADD Wawakumbuka Watoto wenye Ulemavu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika shughuli ya kupokea vifaa vya shule kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo ameagiza mikoa yote kukamilisha uundwaji wa kamati za walemavu kwa ngazi za mikoa, wilaya, […]