Habari za mikoani

RC Shinyanga Awashukia Viongozi na Kuwatimua

Mkuu wa Mkoa Mhe. Zainab Telack akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiangalia uharibifu uliofanywa kwenye vyumba vya madarasa vinavyojengwa baada ya kuchimbwa ili kutafuta madini ya almasi kulikofanywa na wajumbe wa kamati ya shule ya msingi jitegemee kwa kushirikiana na Serikali ya kijiji cha Maganzo Wilayani Kishapu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameivunja Serikali ya kijiji cha Maganzo […]

Habari za mikoani

Mtwara-Mikindani Yatumia zaidi ya Mil. 830 Kutekeleza Miradi ya Maendeleo.

Ujenzi wa Shedi ya Mwalo wa Mikindani, Huu ni Mmoja ya Miradi iliyotekelezwa kwa Fedha hizo.
NaJamadi Omari- H/Manispaa Mikindani

Katika kuhakikisha kuwa Manispaa Mtwara-Mikindani inaendelea kuboresha huduma za Jamii kwa Wananchi wake, imetoa na kutumia fedha kiasi cha shilingi milioni  834,074,361.79 kutoka katika mapato yake ya ndani Kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwepo  kuchangia mfuko wa Wanawake na Vijana pamoja na ulipaji fidia kwa […]

Habari za mikoani

Bolisa Walilia Mitaro kwa TARURA

Hali ya Mitaro katika Barabara ya Bolisa Halmshauri ya Mji Kondoa.
Na. Sekela Mwasubila
Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kutengeneza mifereji pembezoni mwa barabara zilizofanyiwa matengenezo ili kuwa na barabara zinazopitika muda wote.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Bolisa Mh. Abed Boki alipokuwa akiongelea juu ya hali ya barabara ya kuelekea Bolisa kutoka Kondoa Mjini kwa […]

Habari za mikoani

Mhe. Mongella asisitiza ukusanyaji wa Mapato kwa kutumia Mfumo wa kielektoniki

Na Remija Salvatory
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameongoza kikao cha Ushauri cha Mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kujumuisha wajumbe mbalimbali wa kikao hicho ikiwa ni pamoja na Mhe.Waziri wa Kilimo Mifugo  na Uvuvi Mhe. Dkt.Charles, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula, Waheshimiwa Wabunge,Wakuu wa Wilaya,wakurugenzi,Meya wenyeviti na baadhi ya walikwa kutoka Taasisi mbalimbali.
Mhe. Mongella pamoja na kutoa Maagizo mbalimbali kwa watendaji kuhusiana na […]

Elimu

Wizara ya Elimu Yatoa Vitabu 16,985 Kwa Shule za Sekondari Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu Sekondari na baaadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi(hawapo pichani), kabla ya kukabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa maafisa elimu wilaya vilivyotolewa na wadau mbaimbali wa Elimu
 
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Wizara ya Elimu […]

Habari za mikoani

DED Awataka Walimu Kushiki Shughuli za Maendeleo

Na Bathromeo C Chilwa H/W Geita
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ali A. Kidwaka amewataka Walimu na Waratibu Elimu Kata kushiriki kikamilifu zoezi linaloendelea la ujenzi wa miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari katika kata mbalimbali za Wilaya ya Geita ili kuhakikisha tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwa wilaya ya Geita linabaki historia.
Hayo ameyasema wakati wa kikao cha pamoja kati ya Walimu Wakuu wa Shule za Msingi,Waratibu Elimu Kata pamoja na maafisa Elimu ngazi ya Wilaya […]

Afya

Manispaa Yafikia Asilimia 93 Ujenzi wa Kituo cha Afya Likombe

 
Picha ikionesha Jengo la kulaza maiti (Mortuary)
Na Jamadi Omari Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Hadi kufikia Disemba 31,2017 Manispaa ya Mtwara-Mikindani imefikisha asilimia 93 ya ujenzi wa miundombinu ya afya katika kituo cha afya likombe  na kugharimu kiasi cha fedha shilingi milioni  326,457,759.18 kati ya milioni 500 zilizotolewa na Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo.
Asilimia 7 iliyobaki inatarajia kukamilika baada ya wiki […]

Elimu

P4R Yafanya Vizuri Magufuli Sekondari: Prof. Ndalichako

 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bwanga wakati wa Ziara yake Magufuli Sekondari.
Na Magesa Jumapili- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro.Joyce Ndalichako amefanya ziara Wilayani Chato ya kuitembelea Shule ya Sekondari Magufuli na kukagua utekelezaji wa miradi ya lipa kulingana na matokeo(P4R) na kuridhishwa na shughuli zinazo endelea […]