mikoani

Serikali Yaigiza TARURA Kujenga Barabara kwa Wakati

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akitoa maelekezo kwa Watendaji wa TARURA nchini kuacha kutengeneza barabara kama bado haijatengewa bajeti ili kuondoa adha kwa wananchi. Kulia kwake ni Dkt. Binilith Mahenge Mkuu wa mkoa wa Dodoma na kushoto ni Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi, Lusako Kilebwe
Na Fred Kibano
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa […]

Miundombinu

Waziri Jafo Apiga Marufuku Uchimbaji wa Mchanga

Mvua na athari zake katika Jiji la Dsm
Na Raphael Kilapilo, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo (Mb) amepiga marufuku uchimbaji wa mchanga unaoendelea katika mito mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Jafo alitoa katazo hilo wakati wa ziara yake ya kuangalia athari zilizotokana na mafuriko katika Halmashauri ya Manispaa […]

Miundombinu

Waziri Jafo Aigiza TARURA kujenga Barabara ya Chang’ombe – Mipango

Mh. Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais akizungumza na wananchi katika Eneo la Chang’ombe Mkoani Dodoma.
Anaandika  Fredy Kibano OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo, ameagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA) kuelekeza bajeti yao ya mwaka 2018/2019 kujenga barabara ya kilomita  tatu kutoka Kata ya Chang’ombe hadi Chuo […]

Miundombinu

Vituo vya Afya Kanda ya Ziwa vyaboreshwa, Nikumuokoa Mama na Mtoto.

 

Msimamizi  wa huduma za Uuguzi naUkunga  na Mratibu wa  Mradi wa afya ya Uzazi, Mama naMtoto (RMNCH-UNFPA) Bibi. Dinah Atinda akiwa naBiomedical Engineers kutoka Wizara ya Afya Maendeleo yaJamii, Jinsia , Wazee na Watoto wakifunga vifaa katika chumbacha upasuaji katika kituo cha afya cha Iboya Mbongwe Mkoani Shinyanga

Baadhi ya Vifaa vilivyofungwa katika jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Msimamizi  wa huduma za Uuguzi na Ukunga na Mratibu wa  Mradi wa afya ya Uzazi, Mama na Mtoto(RMNCH-UNFPA) Bibi. Dinah Atinda (wa kwanza Kushoto) akikagua baadhi ya vifaa vilivyotolewa na shirika lisilo la serikali UNFPA tayari  kwa kutawanywa katika vituo vya afyaMkoani Shinyanga.
Angela Msimbira
Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la United Nations Population Fund (UNFPA) katikamwaka wa fedha wa 2016/17 mradi wa RMNCH-UNFPA imetumia shilingi bilioni  1.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa  vyaafya katika mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Mwanza kwa lengo la kuboresha vituo vya afya kuweza kutoa huduma za msingi za  katikazahanati (BEmONC) na huduma ya dharura ya afya  ya uzazi ya mama na watoto wachanga katika  vituo vya afya ( CEmONC).
Hayo yamesemwa na msimamizi  wa huduma za Uuguzi naUkunga  na Mratibu wa  Mradi wa afya ya Uzazi, mama namtoto (RMNCH-UNFPA) Bibi. Dinah Atinda wakati wa ziaraya kufanya tathimini ya awali ya kukagua vituo vya afya nazahanati ambavyo vimetengewa fedha jumla ya shilingi bilioni2.8 kwa ajili ya ukarabati/ujenzi katika mwaka wa fedha2017/2018 katika Mkoa wa Simiyu ili viweze kutoa huduma zamsingi na dharura za  afya  ya uzazi ya mama na watotowachanga  katika  vituo vya afya na zahanati.
Bibi. Dinah Atinda amesema utekelezaji wa mradi wa RMNCH-UNFPA ulianza kutekelezwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana naShirika lisilo la kiserikali (UNFPA) mwaka 2015 katika Mikoamitano (5) ya kanda ya ziwa .
Akifafanua zaidi amesema hadi kufikia julai, 2017 Mradi waAfya ya uzazi , mama na mtoto (MRNCH-UNFPA) Kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa umewezakujenga visima virefu vya maji na kukarabati wodi za wazazikatika vituo vya afya vya BWANGA(Chato), kituo cha afya cha Nzera (Geita), Ujenzi wa benki salama za damu mbili(2)zilizopo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga naujenzi wa jengo la  upasuaji Mkoani Kagera, Ujenzi wa majengoya upasuaji (4) katika vituo vya afya  Iboya iliyopo wilaya yaMbogwe, Bwanga iliyoko wilaya Chato,   Uyovu iliyoko wilayaya Bukombe, Kituo cha Afya cha Magoto iliyopo wilaya yaTarime, Kituo cha afya cha Kinesi katika wilaya ya Lorya, Kituocha afya Maruti na Kagunguli  zilizoko wilaya ya UkereweMkoa wa Mwanza.
Bibi. Dinah Atinda amesema pamoja na ujenzi /ukarabati huomradi umeweza kununua vifaa  na kuvisambaza, kuvifungakatika vituo 8 vilivyokarabatiwa ikiwa pamoja na kuwafundishawatumishi jinsi ya kuvitumiakwa kushirikiana na Wizara yaAfya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto. Baadhi yana Vifaa hivyo ni mashine za kutolea dawa za usingizi(Anaesthesia mashine) Oxygen Concentrator, vitanda vyakufanyia upasuaji, vitanda vya kujifungulia , vitanda vyawagonjwa, “Pulseoxynometer ” mashine ya kutakasa vifaa vyaupasuaji “Autoclave” machine”, “infant wormers”, “Incubators”, “stretchers”, monitor, friji za chanjo na maabara, taa za kufanyiaupasuaji, na troly.
Amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 Ofisi ya RaisTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Kupitia ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali UNFPA imepangakukarabati vituo vya afya sita, zahanati 28 ,ununuzi wa magari 3 ya kubebea wagonjwa na magari sita ya kuratibu wa shughuliza mradi katika Mkoa wa Simiyu.
Amesema wamechagua Mikoa ya kanda ya Ziwa kutokana namatokeo ya utafiti uliofanyika mwaka 2015 na kuonyesha  kuwaMikoa hiyo ndio ilikuwa na idadi kubwa ya vifo   vyawajawazito, idadi kubwa ya mimba za utotoni, miundombinuhafifu ya afya na idadi kubwa ya akina mama kujifungulianyumbani na upungufu mkubwa wa vifaa vya CEmONC naBEmONC.
Aidha amesema kuwa serikali imejiwekea lengo la kuhakikishakuwa vituo vya afya vya mikoa ya kanda ya ziwa vinawezakutoa huduma za mssingi na dharura katika Zahanati na vituovya afya ili kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto nakupunguza magonjwa na vifo vitokanavyo na Uzazi.