Video

Sijaridhika na Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Chamwino – Jafo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo pamoja na uongozi wa mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino akiangalia ukubwa wa zege la msingi kwa kutumia ‘tape’ na unyoofu wa zege la msingi kwa kutumia pima maji huku fundi akiweka vipimo hivyo alipofanya ziara ya kujionea ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Na Fred Kibano
Waziri wa […]

Miundombinu

Serikali Yaigiza TARURA Kujenga Barabara kwa Wakati

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akitoa maelekezo kwa Watendaji wa TARURA nchini kuacha kutengeneza barabara kama bado haijatengewa bajeti ili kuondoa adha kwa wananchi. Kulia kwake ni Dkt. Binilith Mahenge Mkuu wa mkoa wa Dodoma na kushoto ni Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi, Lusako Kilebwe
Na Fred Kibano
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa […]

Video

TAMISEMI yaandaa mwongozo mpya wa usimamizi wa mapato kwa Halmashauri

Na Mathew Kwembe
Serikali imesema kuwa mwongozo mpya wa ukusanyaji mapato katika halmashauri unalenga kuongeza wigo wa makusanyo ya mapato kwa kuwatoza watu wengi badala ya wachache na hivyo kuziwezesha halmashauri kukusanya mapato mengi zaidi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Beatrice Njawa mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili Mwongozo wa Usimamizi Ukusanyaji Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi […]

Video

Sera mpya ya Ugatuaji wa Madaraka kuzipa nguvu ya kiuchumi Serikali za Mitaa

Na Mathew Kwembe
Serikali imesema kuwa sera mpya ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi imezingatia katika kuzipa uwezo zaidi wa kiuchumi Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutekeleza ipasavyo majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.
Sera hiyo ya Ugatuaji wa Madaraka inatarajiwa kuibadili sera ya sasa ambayo iliandaliwa takribani miaka 20 iliyopita, ambayo kutokana na mazingira ya sasa serikali imeona ipo haja ya kuibadili ili iendane na matarajio ya nchi ya kufikia maendeleo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Akifungua kikao cha […]

Video

Sekta binafsi zatakiwa kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza bidhaa za afya

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akifunga Mkutano wa Tano wa wadau wa afya Nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar-es-salaam.
Angela Msimbira OR-TAMISEMI Dar-es-salaam
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Josephat Sinkamba Kandege ametoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta […]

Video

Mapato ya Hospitali Kondoa Mji yaboresha huduma za Maabara

Mwonekano wa ndani wa jengo la maabara ya Kondoa Mji baada ya kufanyiwa ukarabati
Na. Sekela Mwasubila.
Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kondoa imekarabati jengo la maabara hali iliyopelekea kuboreshwa kwa huduma za vipimo katika hospitali hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Eusebi Kessy alipokuwa akiongelea ukarabati wa maabara hiyo ofisini kwake hivi karibuni.
Alisema kuwa ukarabati huo umefanyika […]

Video

TAMISEMI Yaendelea Kuwabaini Watoto Wenye Mahitaji Maalum

Na. Fred Kibano
Mratibu wa Sehemu ya Elimu Maalum Ofisi ya Rais TAMISEMI, Julius Migea amesema Serikali imeanzisha Mpango wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wenye mahitaji maalum ili kuwabaini na kuwawezesha kumudu stadi hizo muhimu kwa maendeleo yao na Taifa.
Migea aliyasema mjini Dodoma wakati wa kuanza rasmi kwa zoezi hilo lenye lengo la kuwabaini watoto wenye mahitaji maalum kama uoni hafifu, viungo vya mwili, kutosikia, kushindwa kuongea na matatizo mengine.
“Mpango huu wa kukuza stadi za Kusoma, […]

Video

Mhe. Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Mpwapwa

Na. Fred Kibano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Leo Tarehe 6 April 2018, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Maje kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
Taarifa ua utenguzi huo imetolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Alhaji Mussa Iyombe mjini Dodoma,
Utenguzi wa Mohamed Maji unafuatia taarifa iliyotolewa na Tume iliyoundwa kukagua utendaji wake wa kazi na kubaini kuwa ameshindwa kusimamia na kudhibiti mapato ya Halmashauri hivyo kupelekea upotevu wa […]