Habari za mikoani

DC Kilosa : Baraza ndio Chachu ya Maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya kiosa Adam Mgoi, moja ziara Wilayani humu akiangalia shughuli zinazofanywa na wahitimu wa VETA. (Picha na Maktaba ya OR TAMISEMI)

Na Gladys Gabriel H/ W Kilosa.
Baraza la biashara limetajwa kama chachu ya ukuaji wa ujasiriamali na ukuwaji wa uwekezaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Idd Mgoi amesema kuwa, hakuna pingamizi kwamba Baraza la Biashara ni chachu muhimu ya ukuaji wa ujasiriamali na uwekezaji ambao utawezesha kukua kwa uchumi wa Halmashauri ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro; na Taifa kwa ujumla.
”Kwa mujibu wa Sera ya Viwanda, Sekta Binafsi ni injini ya ukuaji wa uchumi nchini, kwa mantiki hiyo wajibu wa pande zote mbili yaani Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana katika kufanikisha azma ya kujenga uchumi imara” amesema Mgoi.
Mgoi amesema shabaha ya Serikali ni kuhakikisha mazingira rafiki na wezeshi ya kufanya biashara na uwekezaji yanaboreshwa kwa kuhakikisha miundombinu ya uendeshaji wa biashara na uwekezaji ipo nani rafiki kwa kila mmoja.
Ameongeza kuwa, Kutoa mrejesho wa mabadiliko yoyote ya kanuni na sheria ndogo kwa Sekta binafsi na kufanya marekebisho ya kanuni au sheria ndogo zinazoainishwa kama ni kikwazo kwa uwekezaji au uendeshaji biashara’’. Ameongeza Mgoi
Katika kuunga juhudi ya Serikali ya awamu ya tano kuhusu mapinduzi ya viwanda Wilaya hiyo imejizatiti kuwa na viwanda vipatavyo 37 ndani mwaka mmoja kutokana na fursa nyingi zilizopo kwenye Wilaya hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *