Habari za Wizara

Dmdp Yaleta Mabadiliko Jijini Dar es Salaam

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Mratibu wa Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Eng. Davis Shemangale(aliyesimama) akifungua kikao cha mapitio ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dmdp) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Lapf Jijini Dar es salaam.

Msimamizi Kiongozi wa DMDP toka Benki ya Dunia Erick Dickson (aliyesimama) akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao cha mapitio ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dmdp) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Lapf Jijini Dar es salaam.

 

Mkurugenzi wa Utawala OR-TAMISEMI Ndg. Mrisho Mrisho(kwanza kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA Ndg. Erick Kitali wakati wakifuatilia kikao cha mapitio ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dmdp) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Lapf Jijini Dar es salaam.

Katika Picha ya pamoja ni baadhi ya viongozi na watalaam wa Ofisi ya Rais TAMISEMI wakiwa na wataalam toka Benki ya Dunia wakati wa ufunguzi wa kikao cha mapitio ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dmdp) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Lapf Jijini Dar es salaam

Wakati utekelezaji wa mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam(Dmdp) ukiwa umefikia nusu katika awamu ya kwanza 2015/16-2020/21 mafanikio yameanza kuonekana kwa kiasi kikubwa ambayo moja kwa moja yanampunguzia changamoto mwananchi wa Dar es salaam.

Akizungumza katika kikao cha mapatio ya utekelezaji wa mradi kinachoendelea JIjini Dar es salaam Mratibu wa miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandishi Davis Shemangale amesema kwa kipindi cha miaka takribani mitatu ya utekelezaji wa mradi huu umetekelezwa kwa mafanikio kwa kuwa malengo yaliyowekwa yamefikiwa.

Shemangale amesema kuwa kupitia mradi huu baadhi ya mitaa sasa inaweza kuwasiliana kwa urahisi zaidi kwa kuwa imeunganishwa na mtandao mzuri wa barabara, foleni zinaendelea kupungua sababu barabara za mrisho zimetengenezwa na zinapitika kwa urahisi, mfumo wa mawasiliano umeboreshwa na usalama wa mitaa umeimarishwa kwa barabara zote zilizojengwa kupitia mradi kuwekwa na Taa.

“Mradi huu ukiwa unaakisi Mpango wa Taifa wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini umeweza kutoa ajira za moja kwa moja kwa wakazi wa Jiji hili kupitia shughuli mbalimbali za mradi zinazoendelea na pia kutengeneza mazingira bora na rafiki kwa wananchi kuweza kujiajiri na kujipatia kipato alisema Shemangale”.

Aliongeza kuwa mradi umefanikiwa kujenga madaraja, vivuko, kingo za mito, pamoja na mifereji ya kusafirishia mvua kwa kiasi kikubwa imeweza kupunguza athari za mafuko katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es saalam.

Aidha Mhandishi Shemangale alizungumzia malipo ya fidia kwa wananchi walioathirika na mradi katika Manispaa za Ilala na Kinondoni kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imekwisha hakiki madai hayo na wakati wowote waathirika watalipwa fidia.

Msimamizi Kiongozi wa DMDP toka Benki ya Dunia Erick Dickson amesema amejionea mwenyewe mafaniko ya mradi na faida zinazopatokana lakini pia amesisitiza zaidi kuzingatia zile athari zinazoweza kutoka wakati wa utekelezaji wa mradi na kujali muda ili kazi zote za mradi ziweze kutekelezwa kwa ubora unaotakiwa.

Mradi wa DMDP, unatekelezwa na Serikali katika Halmashauri tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni ili kukabiliana na changamoto ya ubovu wa miundombinu.

Benki ya Dunia imetoa mkopo nafuu kwa Serikali wa USD 300 Milioni ambazo ni takribani Tsh. Bil 660 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na Shirika la Maendeleo la Nchi za Nodric limetoa USD Mil. Tano (5) ambazo ni ruzuku kwa Serikali kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Aidha Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la “DFID” limechangia ruzuku ya USD Mil. 20 katika kuboresha Bonde la Mto Msimbazi chini ya Mpango wa ‘Tanzania Urban Resilience Programme’.

Serikali ya Tanzaia inachangia Dola milioni 25.20 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi watakaoathirika na mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *