Habari za Wizara

Jafo afurahishwa na ubora wa viwango vya ujenzi wa miradi ya maendeleo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akisoma uzito wa mtoto katika kliniki ya watoto kituo cha afya Buzuruga na anayeshuhudia pembeni yake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John V.K. Mongella wakati alipofanya ziara yake ya kikazi hivi karibuni Mkoani Mwanza.

Mwandishi wetu, Mwanza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Selemani Jafo amezipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya  Ilemela  Mkoani Mwanza  kwa usimamizi  mzuri  na ubora wa viwango vya ujenzi wa miradi ya maendeleo Mkoani hapo.

Mhe. Jafo ametoa pongezi hizo kwenye ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mwanza ambapo alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri za Wialaya ya Nyamagana na Ilemela Mkoani Mwanza.

Mhe Jafo aliwapongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kusimamia vizuri ujenzi wa jengo la Ofisi la Halmashauri hiyo huku akiwasisitiza wakala wa majengo Tanzania kukamilisha ujenzi kwa kuongeza kasi kadri ya mkataba.

Wakati huo huo, Mhe. Jafo alipata wasaa wa kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ilemela ambayo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 1.5, kati ya hizo shilingi milioni 500 tayari zimeshapokelewa.

Sambamba na hilo, Mhe. Jafo alikagua ujenzi wa kituo cha afya cha  Buzuruga ambacho kilipokea jumla ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akina mama, maabara, chumba cha  upasuaji, mochwari na nyumba ya mtumishi.

Aidha, Mhe. Jafo alikagua ujenzi wa kipande cha barabara ya Sabasaba –Kisele- Buswelu yenye urefu wa kilomita tisa (Km 9.7) iliojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 13 zilizotolewa na benki ya dunia.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John V.K. Mongella na na Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula waliishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi makini na madhubuti wa Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi na kuwaletea maendeleo wanayoyataka kwa wakati muafaka kama ilivyoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelezo ya Wakili Kibamba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya fedha na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ilemela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *