Afya

Jafo ashangazwa na kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze

                                     Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akiwasilisha katika kituo cha Afya Mkonze kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaf(Mb)  akitoa maelekzo kwa Mhandisi wa Jiji la Dodoma Ludigija Ndatwa kuhakikisha kituo hicho kinakamilika ifikapo Juni,30 2019

 

Muoenekano wa baadhi ya majengo yanayoendelea kujengwa katika kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze kilichopo Jijini Dodoma

 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekasirishwa na kasi isiyoridhisha ya ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma.

Waziri Jafo ameonyesha hali hiyo wakati alipotembelea KItuo cha Afya Mkonze kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimepokea fedha za ujenzi Tsh. Mil 400 mapema mwezi Disemba, 2018.

“Sikutegemea kukuta kituo cha Mkonze kikiwa katika hali hii, kituo hiki ni miongoni mwa vituo vilivyopelekewa fedha mapema tu na kiko mjini tena Makao Makuu ya Nchi mnashindwa na Halmashauri ambazo ziko pembezoni huko na zina changamoto nyingi lakini wameshakamilisha ujenzi nini kinakwamisha ujenzi wa kituo hiki.

Kituo hiki cha Mkonze kilitakiwa kiwe cha mfano, ujenzi ukamilike mapema kwa sababu kila kitu kiko karibu yenu, vifaa vya ujenzi  mnavipata kwa urahisi, hakuna changamoto ya usafiri ili mfike hapa hata Ofisi ya TAMISEMI iko hapa hapa sasa endapo mmekwama kitu mna njia nyingi za kutatua nashindwa kuelewa kwanini mpaka leo bado mnasua sua kukamilisha ujenzi wa kituo hiki” alisema Mhe. Jafo.

Waziri Jafo aliongeza kuwa Wananchi wanataka huduma za Afya  hawataki  hadithi  Mnatakiwa kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha majengo yote yanayotakiwa tena kwa ubora wa hali ya juu na ifikapo Juni, 30 kituo hiki kikwe kimeshakamilika.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema kuwa fedha walizopokea ni Tsh Mil 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho lakini kutokana na hadhi ya Jiji waliona watafute fedha zaidi ili kufanya Kituo hicho kiwe na ubora sawa na vituo vingine vilivyojengwa Jijini Dodoma.

“Tumeongeza Tsh Mil 100 kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri sasa fedha hizi zilichelewa kubadilishiwa matimizi kwenye bajeti “Realocation” hiyo ndiyo sababu pekee iliyopelekea kuchelewa kwa baadhi ya kazi za ujenzi katika kituo hiki cha Mkonze;

Lakini kwa sasa tumeshafanikiwa kuhamisha izo fedha na tumepokea maelekezo na tutasimamia kuhakikisha kituo hiki kinakamilika ndani ya muda uliopangwa” Alisema Kunambi.

Ofisi ya Rais Tamisemi inatekeleza Mpango wa Maboresho wa Huduma za Afya ambapo Vituo vya kutolea huduma za Afya 352 vipo katika hatua mbalimbali zaukarabati, ujenzi na ukamilishaji. Kazi hii imefanyika kwa awamu tano.

Kati ya hivyo 304 ni Vituo vya Afya ambavyo vitatoa huduma za dharura ya upasuaji kwa mama mjamzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *