Jafo Ateta na Wazee, Aiasa Jamii Isiwadhulumu Maisha.

Naibu  Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizindua rasmi Maadhimisho ya siku ya wazee yaliyozinduliwa kitaifa katika viwanja cha Nyerere Square Mkoani Dodoma.

Na Atley Kuni- TAMISEMI

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo, ameteta na Wazee nchini ikiwa ni siku ya maadhisho ya Wazee Duniani yaliyofanyika Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na maelfu ya wazee kutoka pande zote za nchi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Jafo ameiasa jamii kuwalinda na kuwapenda wazee ambao amewataja kama tunu ya Taifa.

“Nichukue fursa hii kuiasa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanawalinda wazee katika maeneo yao na hasa dhidi ya watu wasiowema ambao wamekuwa wakidhulumu maisha ya vikongwe kwa kisingizio cha Imani za kishirikina.” Amesema Jafo

Mzee Kachenje akitoa neno la shukrani katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.
Baadhi ya wazee waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani
Baadhi ya wazee waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *