Habari za Wizara

Jafo atoa Neno kwa Plan International

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) akifunga warsha ya Shirika la Plan International ya kufanya tathimini na kuweka mipango ya Shirika hilo inayofanyika Jijini Dodoma

Wataalam wa Shirika la Plan International wakiendelea na warsha ya tathimini na kuweka malengo ya Shirika hilo inayofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) katika picha ya pamoja na Meneja wa Uniti ya Kisarawe katika warsha ya Shirika la Plan International inayofanyika Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) katika picha ya pamoja na wataalam wa shirika la Plan International baada ya kufunga warsha ya tathimini na mipango

Meneja Ufadhili wa Plan International Nicodemus Gachu akitoa mada kwa washiriki wa warsha ya tathimini na mipango ya Shirika la Plan International

 

UJENZI wa jengo jipya la ghorofa mbili za Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI linalojengwa katika mji wa serikali limekamilika kwa asilimia 80.
Hayo yamebainishwa jana jijini hapa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Nyamhanga alipokagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo.

Alisema ujenzi wa jengo hilo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 80 na linatarajia kukamilika Mei 30 mwaka huu tayari kwa viongozi na wataalamu wa wizara hiyo kuhamia rasimi Juni 1 mwaka huu.

Nyamhanga alisema uhamiaji huo unatokana na kuwa vitu vya msingi katika jengo hilo vitakuwa vimekamilika na kazi ndogondogo za ukamilishaji wake zitakuwa zikiendelea wakati watumishi wako ndani ya jengo.

“ Kwa sasa ujenzi wa jengo letu la ghrofa mbili umekamilika kwa takribani asilimia 80 na linatakiwa liwe liemkamilika mwisho wa mwezi huu, ili kuanzia Juni Mosi basi viongozi na wataalam wanatakiwa kuingia kwa sababu vile vitu vya msingi vyote vitakua vimekamilika.”

Aidha, Nyamhanga alitumia fursa hiyo kuwataka mafundi wanaofanya kazi hiyo kufanya kazi usiku na mchana ili liweze kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Wizara ya Tamisemi ilikuwa ni miongoni mwa wizara tatu ambazo majengo yake hayakukamilika kutokana na kuamua kujenga ghorofa wakitumia mfumo wa force akaunti.

Hata hivyo, kutokana na kutokamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, Rais John Magufuli aliagiza wizara zote bila kujali ukamilifu wa majengo yao.

Rais Magufuli alisema: “ Umeeleza (Waziri Mkuu Kassim Majaliwa) kuwa baadhi ya majengo hayajakamilika mojawapo ni jengo la TAMISEMI, wao waliamua kujenga jengo hilo ambalo liliwachelewesha.

“ Lakini siku ya ofisi umetaja Jumatatu (jana) na yeye (Waziri Sulemani Jafo) akakae kwenye jengo lake hilo hilo, akake humo humo, ili kusudi kuanzia Jumatatu Serikali yote iwe imehamia kwenye ofisi zao. Kwa hiyo viti vile mvihamishe ili wananchi wenye shida waje hapa, ili wabunge wanaokuja kutafuta barabara, waje hapa.

“ Tusipoamua hivyo, tutabaki na majengo huku, ofisi zitakuwa kwingine na mimi nitakachofanya, nikimtafuta (George-Waziri wa Utumishi) Mkuchika nitakuja hapa, sasa nikiambia Mkuchika yuko ofisi nyingine ya Dar es Salaam au wapi huko, ndio nitajua kuwa haya yalikuwa maneno. Mimi ninataka yale tuliyoyaahidi tuyafanye.

Kutokana na agzo hilo, Waziri na manaibu wake, makatibu wakuu na wataalamu walitii agizo hilo kwa kuhamia kwenye mabada yaliyokuwa yanatumika kuhifadhi vifaa vya ujenzi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *