Habari Kitaifa

Jafo Atoa Onyo kali kwa Mtendaji Mkuu wa DART

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Selemani Jafo, akitoa onyo kali kwa Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama Mwendo Kasi DART Lonald Rwakatale alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma leo

 

Na Fred Kibano

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Selemani Jafo, ametoa onyo kali kwa Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama Mwendo Kasi DART Lonald Rwakatale kutokana na kudorora kwa huduma za mabasi hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Jijini Dodoma leo hii, Waziri Jafo amesema kuwa ametoa onyo kali kwa Mtendaji huyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo mzima wa usafiri huo jijini Dar es Salaam na pia akitaka kujua ni kwa nini Wakala huo (UDART) una sua sua kiutendaji .

Jafo amemtaka Bwana Rwakatale kuhakikisha atoe maelezo ya kina kwa nini huduma hizo zinazorota na kusababisha huduma hizo kudorora.

Jafo amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Rwakatale kumsimamia kwa karibu mtoa huduma wa UDART kwa karibu ili kuweza kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wateja ambao ni wananchi.

Amesema kuwa haiwezeka mradi huo wa usafirishani ambao umesababisha kuipatia sifa Tanzania na kupata tuzo kutoka Worthington DC unatiwa dowa na watu ambao wanania ya kuhujumu meadi huo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amemwagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI (ELIMU) Joseph Kakunda kukaa na menejimemti ya UDART na DART hapo kesho ili kuweza kubaini ni kwanini kunajitokeza malalamiko ambayo yanapelekea waendeshaji hao kuzorotesha huduma jijini Dar es Salaam.

Agizo jingine amelitoa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe kufanya uchunguzi wa kina kwa lengo la kubaini ni akina nani wanahujumu shirika hilo ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hilo.

“namwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe kufanya uchunguzi ili kubaini kama kuna hujuma yoyote inayoendelea na kubaini ni akina nani wanafanya hujuma hiyo ili hatua stahiki zichukuliwe” alisema Waziri Jafo

“Wakibainika watu ambao wanafanya hujuma ya kutaka kuua mradi huo wachukuliwe hatua haraka sana ili na hatua za kisheria zichukue mkondo wake” alisisitiza Waziri Jafo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *