Habari za Wizara

JAFO awaagiza watumishi wa umma kusimamia miradi ya maendeleo kwa weledi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akionge kwenye mikutano wa Viongozi na Watumishi wa Wilaya ya Meatu wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Simiyu.

Mwandishi wetu, Meatu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu na kwa weledi miradi inayotekelezwa katika Halmashauri zao.

Mhe.Jafo aliyasema hayo jana Wilayani Meatu wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ambapo alibaini mapungufu mbalimbali katika umaliziaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.

Alisema watumishi  wana wajibu wa kusimamia kwa umakini mkubwa   utekelezaji wa miradi ya maendeleo  kwenye Halmashaui zao ili kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na ubora unaoendana na thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii.

“Inasikitisha kuona baadhi ya miradi ya maendeleo nchini imekuwa  inatekelezwa chini ya viwango jambo ambalo ni kinyume na matarajio ya Serikali, hivyo ni wajibu wa kila Mtumishi wa umma kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi ya maendeleo nchini,” alisisitiza Mhe. Jafo.

Alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli haitomvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa kutimiza wajibu wake wa kuwaletea maendeleo wananchi wanyonge, walalahoi na wavuja jasho wa Tanzania.

Kauli ya Waziri Jafo inafuatia ziara yake ya kutembelea hospitali ya Wilaya ya Meatu ambapo alibaini dosari mbalimbali kwenye umaliziaji wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya hospitali hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo, dosari alizozibaini ni pamoja na milango kutokuwa katika viwango na Uwiano wa vipimo vilivyomo kwenye BOQ na kupelekea milango hiyo kushindwa kufunga sawa sawa.

 

Jengo la Wodi ya Wazazi iliyojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu , Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Sulemani Jafo akikagua chumba cha Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa Mkoani Simiyu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *