Habari za Wizara

Jafo Awakalia Kooni Wahandisi Washauri

Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Kwanza kushoto) akitoa maelekezo wakati wa kukagua ujenzi wa barabara za mradi wa Tscp zinazoendelea kujengwa katika Jiji la Arusha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Katikati) akipokea maelezo toka kwa Mhandisi wa mradi wa Tscp Jiji la Arusha Eng.August Mbuya(Kulia) wakati wa ziara yake Jijini humo kukagua ujenzi wa barabara za mradi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Kwanza kushoto) akimskiliza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel F.Daqarro wakati wa ziara yake kukagua ujenzi wa barabara za Tscp.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(Kwanza kushoto) akimskiliza Mhandisi Mshauri wa Mradi wakati wa ziara yake Jijini Arusha kukagua ujenzi wa barabara za Tscp.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amewataka wahandisi washauri wanaosimamia miradi ya  barabara katika maeneo mbalimbali nchini kuwa upande wa Serikali ili kudhibiti ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa kupitia miradi mbalimbali.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akakagua maendeleo ya ujenzi wa barabara zinajengwa katika Jiji la Arusha kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati “Tanzania Strategic Cities Project(TSCP)’ unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Amesema kuwa Mhandisi Mshauri unapaswa kusimama na Serikali na kutoa ushauri wenye tija utakaoleta matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi  badala ya kuwatetea wamiliki wa kampuni zinazojenga miundombinu hiyo.

‘Serikali imetoa  hela nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye maendeleo hususani ni miundombinu ya barabara hivyo ni vyema sasa wataalam washauri mkawa bega kwa began a Serikali ili kupusha hasara inayoweza kujitokeza huko mbeleni endapo miradi hii isipojengwa kwa kiwango. 

Aidha Waziri  Jafo amesema kuwa hajarithishwa na hali ya uchafuzi wa mazingira kwenye  mitaro mbalimbali ya Jiji la Arusha na kuagiza mitaro hiyo ifanyiwe usafi wa mara kwa mara ili kuhakikisha Jiji linakuwa safi na barabara zinazoendelea kujengwa zinadumu kwa muda mrefu.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo ameugiza uongozi wa jiji hilo kuunda makundi ya wakinamama  ambao wapo tayari kufanya usafi ili kila kikundi kikabidhiwe barabara ambayo wataifanyia usafi na kutunza mazingira  huku wakipata kipato ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

 Jiji la Arusha limepewa Tsh. Bil 22.296 kwa ajili ya ujenzi wa  barabara  zenye urefu wa Km. 12.5, uboreshwaji wa dampo la kisasa la Muriet pamoja na uwanja wa kisasa wa michezo katika shule ya msingi Ngarenaro.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *