Habari za Wizara

Jafo- Nimeridhishwa na Mradi wa Utunzaji Mazingira

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Mhe. Seleman Jafo akisalimiana na Balozi wa Switzerland nchini Mhe.Florence Tinguely Mattli wakati Balozi huyo alipozulu Ofisi hiyo na kuzungumza na ujumbe wa Ofisi hiyo kuhusua suala la Utunzaji wa mazingira na mradi ambao umeanza kutekelezwa katika Vijiji 30 vya Mkoa wa Morogoro

Na. Atley Kuni-Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo, ameridhishwa na mradi wa utunzaji wa mazingira ulioanza unatekelezwa katika vijiji 30 wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kwa ufadhili wa nchi ya Switzeland na kuiomba Serikali ya nchi hiyo kupitia kwa balozi wake nchini Florence Tinguely Mattli, kuona namna mradi huo utakavyo weza pelekwa maeneo mengine nchini.
Akizungumza ofisini kwake, wakati wa ugeni huo Mhe. Waziri amesema Serikali kupitia OR-TAMISEMI, wameridhishwa na jitihada hizo ambazo serikali ya nchi hiyo imezifanya katika kunusuru mazingira ya Wilaya za Mkoa wa Morogoro walizoanza anza nazo
“Katika mazungumzo yetu, tumekubaliana kwamba, sera zilizopo zinazohusu masuala ya mazingira lakini pia utunzaji wa misitu ya asili, wataalam kutoka OR-TAMISEMI kwakushirikiana na wataalam wengine wa wizara za kisekta kuzipitia na kuona kwa jinsi gani ni rafiki na zitaweza kutumika kuupeleka mradi huu sasa maeneo mengine ya nchi” alisema Waziri Jafo.
Waziri Jafo amesema kusudio la mradi huo kupitia Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili (Tanzania Forest Conservation Group-TFCG), umejielekeza katika misitu midogo midogo ya vijiji (Ngitiri) na inayo milikiwa na Vijiji vyenyewe.
Mradi huo wa kuhifadhi Misitu ya Asili, ulianza mwaka 2012 katika Mkoa wa Morogoro, ulikuwa na awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza ilianza Machi, 2012 hadi Novemba, 2015, ikihusisha Vijiji 10 vya Halamashauri ya Wilaya ya Kilosa; na awamu ya Pili ilianza mwezi Desemba, 2015 kwa kuongezea Halmashauri za Wilaya ya Morogoro na Mvomero awamu inayotarajia kukamilika ifikiapo Novemba, 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga kupitia taarifa yake aliyoitoa mbele ya Mhe. Waziri, inaonesha hadi sasa jumla ya Vijiji 30 vinatekeleza mradi huo kwenye Mkoa wa Morogoro ambapo Vijiji 20 vikiwa ni vya Wilaya ya Kilosa na Vijiji 10 katika Wilaya ya Morogoro.
Balozi wa Switzeland nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, alielezea kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassani na wasaidizi wao wote.
Katika hatua nyingine Balozi huyo ameahidi kushirikiana na Tanzania katika suala shughuliza za sekta ya Afya husuan ni kwenye Afya katika Afya Msingi, ambapo alisema watakuwa tayari kuwezesha Vifaa tiba pamoja na eneo la TEHAMA. Kufuatia uamuzi huo Waziri wa Nchi amemuelekeza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga, kuwaita watendaji wa Ofisi hiyo wa Idara za Idara za TEHAMA pamoja na Huduma za Afya ili waweze kulisimamia.
Ujumbe wa Balozi wa Switzerland nchini ulimshukuru Mhe. Waziri kwa kutenga muda na kukutana nao ili kumuelezea dhamira waliyonayo katika suala zima la maendeleo ya nchi hususan ni katika sekta ya Afya na Mazingira nchini.

 

Picha ya pamoja baina ya Waziri wa Nchi na Balozi wa Switzerland, NCHINI, Katibu Mkuu OR-TAMISEMI pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wakiwa katika picha ya pamoja
Kikao pamoja na Waziri kikiendelea wakati wa Balozi wa Switzerland na ujumbe wake walivyozulu ofisi hiyo hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *