Afya

JAFO: Ukamilishaji wa Ujenzi wa vituo vya afya 210 nchini ni wa kihistoria.

Angela Msimbira OR-TAMISEMI ARUSHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa tayari serikali imeshakamilisha  ujenzi wa miundombinu  vituo vya afya 210 na  wakati huohuo vituo vingine  vipo katika hatua za ukamilishaji  na kuwa najumla ya vituo 350 vilivyojengwa  katika Serikali ya awamu ya Tano ya Mhe. John Pombe Magufuli.

Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Murriet na Kaloleni vilivyopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha leo

Amesema vituo vya afya 350 vimejengwa ndani ya miezi kumi na nane (18) ukilinganisha na vituo vya afya 115 viliyokuwa vikitoa huduma ya upasuaji tangu uhuru hadi mwaka 2015 hivyo ni mabadiliko makubwa katika sekta ya afya.

Amewashukuru Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati za Ujenzi na wananchi kwa ujumla  kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya kwa weledi  na kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika kwa wakati na ubora wa hali ya juu.

“Ninawashukuru Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kamati za Ujenzi wa Vituo vya afya, wananchi kwa kuwa kazi kubwa imefanyakika katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini na kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati” Anasema Mhe. Jafo

Mhe. Jafo amekiri kuwepo kwa changamoto za upelekeji wa vifaa tiba kwenye Vituo vya afya vilivyokamilika na kuwaagiza MSD kuhakikisha wanapeleka haraka vifaa tiba kwenye vituo vya afya vilivyokamilika ili viweze kutoa huduma kwa jamii.

“Bado kunachangamoto katika upelekaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyokamilika wakati katika ujenzi wa miundombinu kulikuwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya vifaa tiba amabazo zilipelekwa MSD lakini inasikitisha kila eninapopita kwenye vituo vya afya vifaa tiba bado havijafika, hivyo nawaagiza MSD kuhakikisha wanapeleka haraka vifaa tiba katika Vituo vya afya ili viweze kutoa huma kwa wananchi” Anasisitiza Jafo

Mhe. Jafo anasisistiza kuwa haiwezekani kuwa na miundombinu bora ya afya lakini kunakosekana vifaa tiba jambo ambalo linasababisha kukamisha maendeleo na wananchi kutokupata huduma bora za afya na kwa wakati.

Akiongelea kuhusu changamoto ya Vifaa tiba Mhe Jafo amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa ya uwpo wa vifaa tiba hivyo amewaagiza MSD kuhakikisha wanaweledi ujenzi na ukarabaati wa vituo vya afya nchini na kuwa kazi ya mfano katika ujenzi wa miundombinu ya afya na kuwa kazi ya mfano nchini.

Wakati huohuo Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha  amesema kuwa Ujenzi  na ukarabati wa Kituo cha afya cha  Kaloleni umegharimu shilingi milioni 400 ambapo  hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimi 45 na tayari majengo yaliyojengwa ni  jengo la X-Rays, Jengo la Wazazi na Upasuaji, jengo la Kufulia nguo na ukarabati wa miundombinu.

Dkt. Chacha anasema kwa upande wa Kituo cha afya cha Murriet jumla ya shilingi milioni 700,000 zimetumika katika ujenzi wa jengo la wagonjwa, maabara, Jengo la Wazazi, jengo la upasuaji, Chumba cha kuifadhia maiti,, kichomea taka, Mfumo wa kuifadhia maji taka na ujenzi wa barabara ndani ya site lengo likiwa ni kutoa huduma za afya katika maeneo ya jirani kwa kuzingatia idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia takriban 56401

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *