Michezo

KAKUNDA AAGIZA TARURA KUJENGA BARABARA ZA VIVUTIO VYA UTALII

Na. Fred Kibano

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe. George Kakunda, ameuagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kuweka mipango ya kuboresha barabara zote zinazoelekea kwenye vivutio vya utalii nchini ili kuvitangaza na kuinua uchumi.

Mhe. Kakunda ameyasema hayo leo wilayani Mufindi mkoani Iringa wakati akifunga mashindano ya mchezo wa golf uliofikia kilele katika viwanja vya Unilever Mufindi kama sehemu ya maadhimisho ya utalii yajulikanayo kama UTALII KARIBU KUSINI yaliyozinduliwa mapema mwezi juni mwaka huu.

 “Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wawe na mipango mizuri ya kuboresha barabara zinazoelekea kwenye vivutio vya utalii”

Katika hatua nyingine, Mhe. Kakunda amewaagiza Wakuu wote wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambazo zipo katika mikoa ya nyanda za juu kusini, kushiriki kikamilifu katika kuweka mikakati ya pamoja ya kutangaza fursa za utalii katika mikoa yao ili kuwavutia wawekezaji  katika huduma za kitalii.

“Wakuu wote wa mikoa na Halmashauri zote zilizopo mikoa

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe. George Kakunda, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mikoa ya nyanda za juu kusini na wachezaji wa golf katika viwanja vya Unilever wilayani Mufindi jana

ya ndanda za juu kusini, kushiriki kikamilifu katika kuweka mikakati ya pamoja ya kutangaza fursa za utalii, zilizopo katika mikoa yote ya kanda ya nyanda za juu kusini”

Kakunda amesema kazi ya kuvitangaza vivutio vya utalii inafanyika kwa umahiri na weledi kama inavyoelekeza Ilani ya Chama Tawala inayoitaka Serikali kufungua fursa za utalii nchini kote kwa kuimarisha miundombinu na vivutio vya utalii lengo likiwa kuongeza pato la Taifa na ajira.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mufindi Jamhuri William, amesema lengo la utalii kupitia mchezo wa golf ni kukuza huduma za kitalii ili kuongeza pato la wilaya ya mufindi kwa shughuli za kitalii.

Naye Clement Mshana Mkurugenzi wa kampuni ya Capital Plus International, ambao ni waandaaji wa kampeni ya utalii karibu kusini,  amesema walifanya makubaliano na mkoa wa Iringa kutumia mchezo wa golf katika kuhamasisha utalii katika mikoa saba ya nyanda za juu kusini ili vijulikane na kufikia kiwango cha kimataifa.

Mwakilishi wa wachezaji golf Briason Nyenzo, amesema zipo changamoto kadhaa zinazowakabili kama vile wachezaji wengi hawaji wakati wa mashindano na hivyo kupunguza hamasa lakini pia hali ya hewa ya Mufindi ni baridi sana na pendekezo lao ni mashindano ya mchezo huo kuanza kufanyika kuanzia mwezi wa nane badala ya mwezi juni kama ilivyo sasa.

Maadhimisho ya utalii ‘UTALII KARIBUNI KUSINI’ yanahusisha mikoa saba ya nyanda za juu kusini ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Songwe na Njombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *