Habari za mikoani

KARANTINE YA HOMA NGURUWE – WILAYANI KILOSA

Kufuatia kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya nguruwe unaondelea wilayani Kilosa kupitia kifungu cha sheria namba 17 cha sheria ya magonjwa ya wanyama namba 17 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007, wananchi wote mnakumbushwa kuwa wilaya ipo katika karantini ya ugonjwa wa homa kali ya nguruwe toka tarehe 22/11/2017 hadi hapo mwenendo wa ugonjwa utakapodhibitiwa na hali kuwa shwari.
“Katika kipindi cha karantini ni marufuku kufanya biashara yoyote ya nyama ya nguruwe ndani ya wilaya,marufuku kuchinja nguruwe na kuuza nyama ya nguruwe ndani au kupeleka nje ya wilaya ya Kilosa, marufuku kusafirisha kuingia au kwenda nje ya wilaya ya Kilosa na ni marufuku kuachia nguruwe kuzurura hovyo mitaani/mashambani ndani ya wilaya ya Kilosa”. Ametahadharisha Daktari wa Mifugo Wilaya ya Kilosa Dokta Yuda L.Mgeni.
Aidha Dokta Yuda amezitaja dalili za ugonjwa wa homa kali ya nguruwe ni homa kali, kukosa hamu ya kula na kupumua kwa shida, vipele vilivyovilia damu kwenye ngozi na masikio, ngozi ya tumboni na masikioni kubadilika rangi kuwa ya bluu/zambarau iliyopauka na vifo vya nguruwe walioonyesha dalili za homa kwa muda mfupi, hivyo anashauri wafugaji wote wa nguruwe kuchukua tahadhari juu ya matumizi ya pumba/mashudu au mabaki ya vyakula kulisha nguruwe kwani ugonjwa huo hauna tiba, kupuliza dawa ya kuua vimelea kwenye mabanda yote ya nguruwe yaliyoathiriwa chini ya usimamizi wa Afisa Mifugo na kuwatenga nguruwe wote wanaoonyesha dalili za ugonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *