Habari za mikoani

Kongole Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa Andrea Mwani akiongea wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Mji wa Kondoa.
2 Attachments

Na Sekella Mwasubila H/W Kondoa Mji

Halmashauri ya wa Mji Kondoa imepongezwa kwa kufanya uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi hii ikiwa ni halmashauri ya pili katika Mkoa wa Dodoma miongoni mwa Halmashaurinane za mkoa huo  kufanya hivyo.

Pongezi hizo zilitolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa, Andrea Mwani wakati uzinduzi wa Baraza alioufanya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi Kondoa Mjini.

Alisema uwepo wa baraza hilo likawe chombo cha kusema katika kufikisha matakwa ya watumishi na kuimarisha ushirikiano na mwajili na kwamba, anauhakika katika baraza hilo wajumbe watawasilisha wanayoona yatafaa katika kushirikiana na mwajiri kutatua changamoto za kazini.

”Mnaweza mkaona katika uongozi huu wa awamu ya tano jinsi Mheshimiwa Rais anavyofanya mabadiliko ya kuiendeleza nchi na wakuyafanya haya ni sisi wafanyakazi hivyo kila mmoja awajibike katika eneo lake na kujitathmini ili tuendane na upepo uliopo.”Alisema Mwani

Aidha alisisitiza wafanyakazi kufanyakazi na kutimiza majukumu yao walioajiliwa nayo kwa asilimia zote pamoja na melekezo wanayopewa kwani kwa kufanya hivyo wanamsaidia Mheshimiwa Rais, Mkuu wa Wilaya, Halmashauri na wananchi wanaowahudumia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji Kondoa Msoleni Dakawa alisema kuwa, Baraza limeanzishwa baada ya kuona umuhimu wa wafanyakazi kwa kuwa katika serikali mfanyakazi ndio mzalishaji na mtekelezaji wa maagizo na ahadi zinazotolewa na serikali.

“Niombe kwa wakati mwingine kwa umoja huu tuliouonyesha na vyama vya wafanyakazi tuendelee nao iwe wakati wa shida na raha kwani lengo ni kuhakikisha mambo yanaenda, natumai wajibu wa kupambana kama anavyofanya Mheshimiwa Rais lengo likiwa kuwahudumia wananchi na kuwapatia haki zao watumishi.” Alisisitiza Dakawa

Naye mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi  ambaye ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma Bwana Mchenya John alisema kuwa baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu cha maamuzi kwa halmashauri na kuwataka wajumbe wa baraza kuacha uoga na kujadili mambo yatakayowasaidia kuendesha halmashauri na maslahi ya watumishi.

“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kulitolea maamuzi suala la kikokotoo kwani liliwakatisha taama sana wafanyakazi na nilishakuja hapa mwaka jana nikapata fursa ya kuongea na wafanyakazi na nashukuru walinielewa na kuwa watulivu wakati wote wa mpito hadi Mheshimiwa Rais alipolitolea maamuzi.”Alimaliza Bwana Mchenya.    

Wajumbe wa baraza la wafanyakazi Kondoa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa baraza hilo.

                                                                                                                                                                                                                                                                   

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *