Habari za Wizara

Kwa Heri Mhandisi Iyombe Tutakukumbuka

Na Fred Kibano

 

Katibu Mkuu Mstaafu OR TAMISEMI (kushoto) Mhandisi Mussa Iyombe akimkabidhi baadhi ya nyaraka za makabidhiano Katibu Mkuu OR TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga katika ofisi za OR TAMISEMI Jijini Dodoma

 

Baadhi ya Viongozi wa OR TAMISEMI wakishuhudia makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI Jijini Dodoma. Mhandisi Mussa Iyombe amemaliza muda wake na Mhandisi Joseph Nyamhanga ameanza kutekeleza jukumu la Katibu Mkuu OR TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amemsifu Katibu Mkuu Mstaafu Mhandisi Mussa Iyombe ambapo amemwelezea kama ni mtumishi aliyejituma kwa ajili ya watu.

“Mhandisi Iyombe amefanya kazi kwa weledi, uadilifu na bidii, lakini katika maisha ya kustaafu tutaendelea kukutumia na usichoke”, alisema Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Iyombe anakabidhi ofisi ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI mara baada ya muda wake kumalizika.

Itakumbukwa kuwa Mhandisi Iyombe ameitumikia OR TAMISEMI kwa muds wa miaka mitatu na kuondoa changamoto nyingi zilizokuwa zinaikabili wizara hii ikiwa ni pamoja na malalamiko ya wananchi, hati chafu, matumiszi mabaya ya fedha na rushwa.

Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Naibu Katibu Mkuu Tixon Nzunda, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Mrisho Mrisho na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Theobald Bagandanshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *