Afya

Kigamboni Manispaa kuanzisha Kidato cha Tano

Moja ya Jengo la Maabara ya Sayansi katika Shule ya Sekondari Nguva inayotegema kuchukua wanafunzi wa Kiume wa Kidato cha Tano kwa Mchepuo wa Sayansi kuanzia Julai,2018

                         Korido ya moja ya mabweni katika shule ya sekondari Nguva yatakayotumiwa 

na wanafunzi wa Kidato cha Tano mapema Mwezi Julai,2018

                       Muonekano wa Maabara za Sayansi katika Shule ya Sekondari Nguva,

Kigamboni Dar es salaam

                         Baadhi ya vifaa kwa ajili ya mafunzo kwa Vitendo, Maabara za Sayansi Shule ya Sekondari Nguva, Kigamboni Dar es salaam

Afisa Habari, Manispaa ya Kigamboni

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni  inatarajia kufungua kidato cha tano na sita Julai mwaka huu  katika Shule ya Sekondari Nguva kwa kuwa na wanafunzi 160 wa kiume pekee ikiwa na  michepuo ya PCM,PCB,HGE na EGM.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa  katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari yenye kidato cha tano na sita kwenye Halmashauri, na kutimiza maelekezo ya Serikali kwa kila Halmashauri kuwa na shule ya kidato cha tano na sita,  Manispaa  iliamua kuboresha miundombinu ya Shule ya Nguva  ili iweze kukidhi mahitaji hayo.

Aidha amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa thamani ya shilingi 492,864,576  kwa kushirikiana na Serikali kuu, ambapo  Serikali kuu imeweza kuchangia kiasi cha shilingi 259,000,000 na vyanzo vya ndani vya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ilichangia shilingi 233,864.576.

Mkurugenzi amesema kwamba  ili kuhakikisha Shule ina hadhi ya kidato cha tano na sita kwa mujibu wa vigezo vya wizara, ujenzi wa mabweni mawili kwaajili ya wanafunzi, vyoo, ujenzi wa daharia ambao  bado unaendelea, ujenzi wa madarasa manne na ununuzi wa madawati, ununuzi wa vitanda kwaajili ya mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa maabara ya sayansi na ujenzi wa jengo la utawala linalojengwa kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda vimefanyika .

 Mkurugenzi amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha masomo ya kidato cha tano na sita yanatolewa kwa watoto wanaomaliza kidato cha nne kwa shule  za sekondari za Kigamboni.

Kukamilika kwa mradi kutawezesha  kuongeza idadi ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na sita,kuchochea maendeleo ya elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kutoa fursa pana kwa wanafunzi kujiunga na elimu ya juu.

Ameongeza kuwa ujenzi wa bwalo la chakula litakalowawezesha wanafunzi kutumia kwaajili ya chakula linaendelea kujengwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *