Video

Mhe. Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Mpwapwa

Na. Fred Kibano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Leo Tarehe 6 April 2018, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Maje kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Taarifa ua utenguzi huo imetolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Alhaji Mussa Iyombe mjini Dodoma,

Utenguzi wa Mohamed Maji unafuatia taarifa iliyotolewa na Tume iliyoundwa kukagua utendaji wake wa kazi na kubaini kuwa ameshindwa kusimamia na kudhibiti mapato ya Halmashauri hivyo kupelekea upotevu wa fedha.

“Hadi kufikia robo tatu ya mwaka wa fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imekusanya mapato kwa asilimia 24 tu pamoja na kuwa Halmashauri hiyo ni kongwe yenye vyanzo vingi vya mapato” alieleza katibu Mkuu Iyombe.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na waandishi wa habari kuhusu kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mohammed Majje leo mjini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *