Habari Kitaifa

Mkurugenzi Nkasi Apumzishwa Kazi Kupisha uchunguzi – Waziri Jafo

1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari Mkoani Dodoma kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Mkoani Rukwa.

Angela Msimbira- OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amekupumzisha kuendelea na majukumu na madaraka ya Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Bw. Julios Kaondo, mpaka hapo uchunguzi wa awali wa tuhuma zinazomkukabili utakapokamilika.
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa Habari Ofisnini kwake, Jafo amesema kuwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi huyo kutokana na Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu Na. 4 (1-5) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka na Wilaya) sura 287 kwa mujibu wa Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Mhe. Jafo amesema amechukua hatua hiyo kutokana na tuhuma zinazomkabili za kujihusisha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa zabuni ya Miradi ya Maji na kushindwa kusimamia manunuzi katika utekelezaji wa miradi ya maji, katika kijiji cha Kamwanda Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa huku akiwa ndiye Ofisa Masuhuli wa Halmashauri
Mhe. Jafo amesema mradi huo ulikuwa ukigharimu shilingi bilioni 7 na wenye lengo la kutatua kero ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na kuwaletea maendeleeo wananchi wa wilaya hiyo.
Mheshimiwa Jafo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watumishi wote waliohusika kukwamisha Mradi wa Maji katika kijiji cha Kamwanda Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa ikiwa ni fundisho kwa watumishi wasiowaaminifu na wasiofanya kazi kwa kuzingatia sheria za utumishi wa umma.
“Jiepusheni na tabia ya baadhi ya watumishi walioko katika Wizara mbalimbali kufanya vitendo vya udanganyifu, endapo itagundulika hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika wote”Amesema Jafo
Ametoa wito kwa Wakurugenzi , Wakuu wa Idara, pamoja na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.kwa kushindwa kusimamia hatua za manunuzi.
Aidha amewataka Watumishi wa umma nchini kufuata kuzingatia sheria, Kanuni na Taratibu na miongozo iliyopo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kujiepusha na vitendo vya rushwa katika kuwahudumia wananchi.
2. Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo wakati akitoa taarifa kuhusu kumpumzisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *