Habari za mikoani

“Msiache kupiga Chapa Mifugo” – Ulega

2.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akipiga chapa ng’ombe katika kijiji Mongoroma ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa zoezi hilo katika kijiji hicho

Na. Sekela Mwasubila
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega amewasihi wafugaji wa wilaya za Chemba na Kondoa kuendelea na zoezi la kupiga chapa mifugo yao ili kiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi ya mifugo.
Ulega aliyasema hayo katika kijiji cha Mongoroma wakati wa ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Chemba, halmashauri ya Mji Kondoa na halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ili kukagua shughuli za mifugo ndani ya Wilaya hizo.
“Mifugo inazaliwa kila mwaka hivyo ni wajibu wenu kuendelea na zoezi hilo la upigaji chapa kwakuwa itasaidia kupata takwimu sahihi ambazo zitaisaidia serikali kupanga mipango ya mifugo kwa malisho, miundombinu, madawa na kuwavutia wawekezaji.
Ulega ameongeza kuwa, uwepo wa zoezi hilo pia utasaidia kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ikiwa ni pamoja kuwasaidia wafugaji kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine kwani watakuwa na kibali kinachotambulika kisheria iwapo kutatokea uhaba wa malisho na kuhatarisha hali za marisho ya mifugo yao.
Aidha aliwapongeza viongozi wa wilaya hizo kwa kusimamia vizuri zoezi hilo na wafugaji kujitokeza kwa wingi kupiga chapa mifugo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ina jumla ya Ng’ombe 19800 ambapo hadi sasa jumla ya ng’ombe 16895 wamepigwa chapa sawa na asilimia 82 ya zoezi na katika ziara hiyo Naibu Waziri alipata fursa ya kufungua upigaji chapa katika kijiji cha Mongoroma.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Denis Mosha akisoma taarifa ya zoezi la chapa mbele ya Naibu Waziri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *