Elimu

Mwanza, Iringa zatamba katika Soka

Na Mathew Kwembe
Mashindano ya michezo ya UMISSETA imeendelea kufanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Nsumba na Chuo cha Ualimu Butimba, huku zikishuhudiwa timu za mpira wa miguu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya Iringa na Mwanza ikitoa vipigo vikali kwa wapinzani wao.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo Leonard Tadeo, matokeo ya michezo iliyochezwa tarehe 8 juni,2018 katika uwanja wa Nsumba kwa upande wa soka wavulana yanaonyesha kuwa Tabora iliifunga Rukwa magoli 3-1, Iringa iliifunga Arusha 1-0 na Mwanza waliifunga Pwani 2-0.
Katika mchezo wa soka wasichana Iringa iliibugiza Rukwa kwa magoli 5-0, Mwanza iliifunga Tabora 2-0 na Mwanza waliifunga Rukwa 5-0.
Matokeo ya mpira wa wavu wavulana yanaonyesha Mwanza 3, Rukwa 0, Arusha 3 Tabora 1, Rukwa 0 Pwani 3. Kwa upande wa mpira wa wavu wasichana katavi 15 Tabora, Arusha 23 Iringa 28.
Katika mpira wa kikapu wavulana matokeo yanaonyesha Mwanza 99 Katavi 9, Rukwa 28 Iringa 32, Tabora 38 Arusha 44, Pwani 41 Iringa 21. Kwa upande wa mpira wa kikapu wasichana Katavi 15 Tabora 14, Arusha 23 Iringa 28

Katika mpira wa pete wasichana Iringa 18 Mwanza 26 Katavi 17 Tabora 36
Matokeo ya mpira wa mikono yanaonyesha Pwani 12 Mwanza 20, katavi 15 Arusha 22, Tabora 29 Rukwa 17. Kwa upande wa mpira wa mikono wasichana Rukwa 8 Arusha 8, Mwanza 8 Tabora 7

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *