Naibu Waziri Jafo- “Msifanye Masihara na Fedha za Uboreshaji Vituo vya Afya”

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TANISEMI  Selemani Jafo ((Mb) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni.

Na Atley Kuni- TAMISEMI.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ameonya vikali yeyote atakayethubutu kufanya Masihara na fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya uboreshaji wa Vituo Vya Afya Nchi.

Jafo ametoa onyo hilo mara baada yakutembelea Kituo cha Afya cha Kintinku kilichopo Mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara zake anazo zifanya takribani maeneo yote ya nchi kwaajili ya kuhakikisha fedha zilizo tolewa kwaajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwepo suala la Afya zinatumika kama jinsi ilivyo kusudiwa.

“Uboreshaji huo utajumuisha ujenzi wa chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti, wodi ya kisasa ya akina mama na maabara na kuwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha hadi desemba 30, mwaka huu ujenzi huo uwe umekamilika” amesema Jafo.

Jafo amesema katika awamu ya kwanza jumla  shilingi milioni 500 zimepelekwa kwenye kila kituo kinacho tarajiwa kufanyiwa ujenzi  kwa ajili ya miundombinu na baada ya ujenzi kukamilika serikali itaweka vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 220,nataka ujenzi huu uende kwa kasi atakayeleta masihara atajuta, Ameonya Naibu Waziri Jafo.

Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kama timu moja na ifikapo 30 Desemba, 2017 kazi hiyo iwe imekamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *