Video

Ondoeni Vifo vya akina mama na Watoto- Dkt.Chaula

Na. Fred Kibano

Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula amewataka Wadau wa afya kufuata Sheria, Miongozo na Sera ili kuboresha utendaji katika Sekta ya afya nchini.

Dkt. Chaula ameyasema hayo wakati akiendesha kikao kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadau wa Afya waliohusisha asasi za JHPIEGO, Management and Development for Health (MDH), Health Jonson Foundation MRI Mikoa ya Nyanda za juu kusini na Water Reed Program pia mikoa ya nyanda za juu kusini.

Dkt, Chaula amesema lengo kuu la kikao kazi hicho ni kupitia kazi za Wadau hao ili kuona namna ambavyo wanatekeleza kazi zao lakini kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa kazi za sekyta ya afya nchini.

Wadau hao wanatekeleza kazi zao ambazo zinapatiwa fedha na Shirika la Maendeleo la Marekani USAID/PEPFAR.

Asasi hizo za mfanano zinatoa huduma ya TB, Ukimwi na afya ya mama na mtoto.

Katika hatua nyingine Dkt. Chaula amezitaka Asasi nchini na Wadau katika sekta ya afya kujikita katika kuondoa vifo vya akina mama na watoto badala ya kutaka kuendelea na mpango mpya uliopendekezwa na Wafadhiri.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadau wa Afya nchini wanaohusika na TB na Virusi vya Ukimwi na UKIMWI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *