Elimu

OR TAMISEMI Yaipongeza Hai.

Naibu waziri akizungumza na wanafunzi shule ya Sekondari Harambee

Na. Riziki Lesuya H/W-Hai.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda ameridhishwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo Wilayani Hai huku akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yohana Sintoo kwa usimamizi mzuri unaozingatia thamani ya fedha.

Mh. Naibu Waziri alitoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Wilayani Hai wakati wa kutembelea na kukagua upanuzi wa mradi wa maji wa Losaa-Kia pamoja na ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Harambee.

Naibu Waziri amewapongeza wananchi kwa kuunga mkono juhudi za serikali kupitia michango ya fedha na nguvu kazi katika ujenzi wa bweni kwenye shule hiyo ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Shule hiyo ujenzi wa bweni hilo umegharimu kiasi cha shilingi 200,386,000.

Kwa mujibu wa taarifa imesema kati ya hizo mchango wa wananchi ni shilingi 181,986,000/= michango iliyosimamiwa na serikali ya Kijiji wa eneo hilo.

Sambamba na pongezi hizo Kakunda ameitaka Halmashauri kutumia utaratibu wa ‘force account’ katika utekelezaji wa miradi midogo kwa kuwa uzoefu umeonyesha miradi mingi iliyofanyika kwa utaratibu huo imekamilika kwa wakati na kwa ubora huku ikipunguza gharama za utekelezaji wa miradi.

“Tumieni force account na tumieni mafundi wanaopatikana katika maeneo yenu kwani kazi zao zimekuwa za ubora kwenye maeneo mengi, mkifanya hivi mtakuwa mmetoa ajira kwa wananchi wenu lakini pia mtakuwa mmetekeleza miradi yenu kwa gharama nafuu” alisema Kakunda.

Jengo la bweni Shule ya Sekondari Harambee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *