Mafunzo

Maafisa TEHAMA Wanolewa Mfumo wa Epicor

Na. Fred Kibano
Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanapatiwa mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa epicor ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo hayo baada ya kutolewa kwa wahasibu, waweka hazina na maafisa manunuzi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya epicor 10.2 wakifuatilia mada kwa makini kuhusu maboresho ya mfumo wa epicor, mafunzo hayo yahusiha washiriki kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, […]

Habari za Wizara

Tufanye Kazi Kama Ibada, Jafo

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Watumishi kufanya kazi kama sehemu ya ibada ili waweze kutoa huduma stahiki kwa Wananchi na hatimaye kupata  thawabu kwa Mwenyezi Mungu.
Jafo ameyasema hayo wakati  wa futari maalumu ya pamoja iliyofanyika kwenye viwanja vya Wizara jioni ya leo kwa Viongozi wa Serikali, Wafanyakazi wa Wizara, Taasisi zilizochini ya Wizara, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Taasisi […]

Mafunzo

PS3 yaombwa iende mikoa yote Tanzania Bara

Afisa TEHAMA wa OR TAMISEMI Mfaume Mnokote akiwasilisha mada ya matumizi ya dawati la dharura kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 jijini Mwanza
Atley Kuni na Glady Mkuchu – Mwanza
Washiriki wa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 kutoka mikoa ambayo haitekelezi Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), wameiomba Serikali ione namna itakavyoweza kukaa na […]

Habari za Wizara

Viongozi wa Serikali za Mitaa kuweni chachu ya Mabadiliko, Nzunda

 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akichangia mada kwenye warsha ya namna ya Uendeshaji wa mabaraza ya Biashara kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mradi wa Local Investiment Climate (LIC) iliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi […]

Habari za Wizara

Takwimu sahihi za watu wenye ualbino zitasaidia utoaji wa huduma bora

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akizikiliza jambo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa walemavu wa ualbino wakati wa maadhimisho ya 13 ya Kitaifa na ya 4 Kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Simiyu.
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za […]

Habari za Wizara

Waganga Vituo vya afya, Wakuu wa shule jifunzeni elimu ya uhasibu

Na Mathew Kwembe, Kagera
Waganga Wafawidhi wa Vituo vya Afya, Zahanati na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari wanaopelekewa fedha na serikali moja kwa moja kwenye vituo vyao wametakiwa kujifunza elimu ya uhasibu ili waweze kutekeleza majukumu yao uafisa masuuli ya usimamizi wa fedha za serikali.
Ushauri huo umetolewa jana na Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma wa Mkoa wa Kigoma bwana Simon Mabagala wakati wa mahojiano maalum kuelezea alichojifunza kuhusu watendaji hao wa ngazi […]

Elimu

Mwanza, Iringa zatamba katika Soka

Na Mathew Kwembe
Mashindano ya michezo ya UMISSETA imeendelea kufanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Nsumba na Chuo cha Ualimu Butimba, huku zikishuhudiwa timu za mpira wa miguu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya Iringa na Mwanza ikitoa vipigo vikali kwa wapinzani wao.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo Leonard Tadeo, matokeo ya michezo iliyochezwa tarehe 8 juni,2018 […]

Elimu

Kakunda ahimiza halmashauri ziwekeze kwenye michezo

Na Mathew Kwembe, Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe. Joseph Kakunda amesema wakati umefika sasa kwa Halmashauri kupitia mabaraza yao ya madiwani kutenga fedha kwenye bajeti zao kuwekeza kwenye sekta ya michezo.
Mhe.Kakunda ameyasema hayo hivi karibuni jijini Mwanza kwenye ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ambapo alieleza kuwa halmashauri kupitia mabaraza ya madiwani zina fursa ya kuwekeza kwenye michezo kwani ni njia mojawapo ya kuinua uchumi wa halmashauri zao na taifa.