Video

Sekta binafsi zatakiwa kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza bidhaa za afya

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akifunga Mkutano wa Tano wa wadau wa afya Nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar-es-salaam.

Angela Msimbira OR-TAMISEMI Dar-es-salaam

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Josephat Sinkamba Kandege ametoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya afya  hasa kwenye viwanda vya kutengeneza  bidhaa za afya nchini.

Ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa Tano wa wadau wa Sekta ya afya nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar-es-salaam.

Mhe. Kandege amesema kuwa Tanzania  kwa sasa kuna makampuni 14  yanayojishughulisha na bidhaa za afya (Dawa, Vifaa, vifaa tiba na  vitenda) yenye mtaji mdogo ukilinganisha na mahitaji ya huduma hiyo nchini hivyo ni vyema makampuni binafsi yakawekeza ili kukidhi mahitaji ya nchi.

Mhe. Kandege amewataka wawekezaji wenye nia ya dhati  kuja kuwekeza kwenye makampuni  ya kutengeneza  bidhaa za afya hasa watanzani  wenye uwezo wa kifedha  kutumia nafasi hii adimu kuwekeza nchini.

Amesema kuwa Kasi ya makampuni ya wazawa kuwekeza katika viwanda vya bidhaa za afya  nchini hayaendani na uhitaji  halisi kwa sasa kwa kuwa nchi huagiza  asilimi 94 kutoka nje.

Amesema kuwa sekta ya afya ni muhimu katika jamii hivyo ni vyema  mshirika binafsi kuhakikisha wanawekeza katika sekta ya afya  hasa katika viwanda vya madawa kwa kuwa uhitaji wa dawa nchini ni mkubwa  ukilinganisha na uzalishaji wa bidhaa hizo nchini.

Mhe. Kandege amesema kuwa Tanzania  inatumia  zaidi ya shilingi trilioni  moja ( trilioni 1 )  kila mwaka  katika masuala ya afya lakini  ni asilimia kumi ndio hutumika katika viwanda vya ndani.

Wakati huohuo rais wa chama cha wadau wa Afya nchini  Dkt. Omary Chilo amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya nchini ambapo  maendeleo ya viwanda Tanzania  na changamoto ya nini kifanyike katika kuwekeza katika viwanda upande wa sekta ya afya.

Amesema maendeleo ya viwanda katika sekta ya afya ni jambo la muhimu kwa kuwa teknolojia imebadilika  na magonjwa yanayobadilika  hivyo viwanda katika sekata ya afya imebadilika katika sehemu kuu nne ambapo viwanda vya madawa, viwanda ambavo vinahusisha kutengeneza vifaa tiba na kuwekeza katika rasilimali watu

Amesema kuwepo na viwanda vya kutengeneza bidhaaza afya (Dawa,vifaa, vifaa tiba na vitenda) kutasaidia  kupunuza bei ya madawa  ambazo zitamsaidia mwananchi maskini , kuongeza ajira kwa wananchi na ushindani kuongezeka ili kuleta tija katika kukuza uchumi wa nchi katika sekta ya afya.

Aidha  amesema kuwa dunia imekuwa kama kijiji kwa kuwa hakunakitu kinachoweza kufanyika bila kuwa na takwimu sahihi, hivyo ni vyema kukawa na mkakati wa kukusanya , kuingiza  na kuifadhi na jinsi ya kutumia takwimu mbalimbali ili kuboresha afya nchini.

Rais wa Chama cha Wadau wa Afya Nchini Dkt. Omary Chilo akipatiwa maelezo katika Banda la maonesho la Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika Mkutano wa Tano wa Wadau wa Afya Nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar-es-salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Tano wa wadau wa afya Nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat  Sinkamba Kandege alipokuwa akifunga mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar-es-salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *