Habari za Kijamii

Serikali yakabidhi mchango wa matibabu kwa kijana Gabriel

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ELIMU (OR TAMISEMI) Mhe. Mwita Waitara akikabidhi mchango wa shilingi milioni tisa kwa kijana Gabriel Amos uliochangwa na watumishi ngazi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mikoa na Halmashauri Jijini Dar es Salaam leo
Kijana Gabriel Amos aliyepata ulemavu baada ya kudondoka kutoka mtini akiwa shuleni Samora Machel mkoani Mbeya ambako alikuwa akisoma kidato cha pili akitoa shukrani kwa Serikali na wote waliompatia msaada

Na Rebecca Kwandu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ELIMU (OR TAMISEMI) Mhe. Mwita Waitara amekabidhi mchango wa shilingi milioni tisa kwa kijana Gabriel Amos uliochangwa na watumishi ngazi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mikoa na Halmashauri Jijini Dar es Salaam leo.

Mhe. Waitara amekabi mchangohuo kwa Kijana Gabriel Amos aliyepata ulemavu baada ya kudondoka kutoka mtini akiwa shuleni Samora Machel mkoani Mbeya ambako alikuwa akisoma kidato cha pili mapema mwaka huu.

Akikabidhi mchango huo kwa kijana Gabriel Amos nyumbani kwao Mbagala Kizuiani Jijini Dar es Salaam Mhe. Waitara amesema kuwa tumwombee Gabriel kwa Mungu ili apate nafuu haraka na kuendelea na masomo yake kama alivyotarajia.

 “sote tumwombee kwa Mungu amponye Amos ili hatimaye aweze kuendelea na masomo yake na hatimaye kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari. Huwezi kujua kwanini hili limetokea na huenda ikiwa ndiyo njia ya kupatikana kwa mambo mengi” Alisema Waitara.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkabidhi mchango huo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Mhe. Waitara, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Tixon Nzunda, amesema mchango huo uliotolewa ni wa awali na kwamba anatoa wito kwa mtu yeyote kuendelea kumchangia mtoto kijana Amos bila kikomo kwani bado anahitaji fedha za matibabu Zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Temeke Mhe. Felix Lyaniva ameahidi kupeleka gari la kumchukua mtoto kijana Amosi na mama yake kila siku asubuhi kwa kipindi ambacho atakuwa akihudhuria matibabu yake.

Naye kijana Gabriel Amos ameishukuru Serikali kwa msaada iliyompatia na kuiomba jamii kuendelea kumchangia kwa sababu matibabu yake yanahitaji fedha nyingi.

Shughuli ya makabidhiano ya mchango huo imehudhuriwa na Afisa Ellimu Mkoa wa Dar es Salaam, Waratibu Elimu Kata, Wathibiti Ubora, Mtendaji wa Kata ya Kizuiani, ndugu wa Amos na baadhi ya majirani. 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *