Habari za Wizara

Simamieni nidhamu mashuleni kuleta mabadiliko

 

Naibu Katibu Mkuu Elimu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Tixson Nzuda akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi (hawapo pichani) kwenye kikao kazi cha kujadili muelekeo wa masuala mbalimbali ya maendeleo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Elimu  Tickson Nzunda amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanasimamia maadili, utoro na uwajibikaji wa waalimu na wanafunzi ili kuweza shule zinazomilikiwa na Serikali ziweze kushindana katika ufaulu na shule binafsi nchini

Ameyasema hayo wakati akiongea na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi kwenye kikao kazi cha kujadili muelekeo wa masuala mbalimbali ya maendeleo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Nzunda amesema kuwa  ili   kuweza kuwa na uimara  katika shule za Serikali  ni lazima kukawa na mpango maalumu wa kuimarisha shule za Serikali kwa kuzijengea heshima ili ziweze kupambana katika ubora na ufaulu na shule binafsi.

Anaendelea kufafanua kuwa Makatibu Tawala wa Mkoa na Wakurugenzi wote nchini wanatakiwa kuhakikisha kila shule inakuwa na mpango Mkakati ili kujua muelekeo wa malengo yaliyopangwa na serikali katika kutimiza majukumu ya kila siku ya shule zao.

Awataka kuhakikisha wanasimamia ufundishaji na ujifunzaji  kwa  kuwajenga  waalimu kuwa wabunifu na kuwapa fursa ya kupanga wenyewe wanayofundisha  ili kuwapima kutokana na matokeo wanayayafanya. Pia wahakikishe wanaimarisha  uongozi wa shule ili  kuongeza kasi ya ufaulu kwa wananfunzi.

Amefafanua  kuwa ili kuweza kufanikiwa katika suala zima la Elimu nchini ni lazima viongozi hao wakahakikisha  wanaimarisha bodi za shule  kwa kuwa bodi hizo ndizo muhimili mkuu wa Shule na  ndio wanaopanga mikakati  itakayotekelezwa ili kuleta maendeleo ya shule hizo.

Nzuda amesema ni vyema wakahakikisha waalimu wanafudisha kwa kutumia zana za kufundishia kwa kuzingatia mazingira yanayowazinguka  na kuhakikisha wanawatia moyo waalimu wanaofaya vizuri kwa kuwapogeza hata kwa kuwaandikia barua kwa kazi nzuri wanazozifanya ili  kuchochea mwamko wa  kufundisha kwa umakini zaidi.

Ameendelea kusisitiza  kuwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuhakikisha wanajenga msingi mzuri wa Elimu ya Msingi , kwa kudhibiti waalimu na wanafunzi watoro darasani  kwa kuwa fursa nyingi hazipatikani mashuleni kutokana na mdondoko wa wanafunzi nchini na kuleta matokeo mabaya katika shule za Serikali.

“Tumefaya utafiti  na kugundua kuwa  kila siku  katika kila shule asilimia 12 ya waalimu ni watoro mashuleni , hivyo wakurugenzi mnatakiwa kudhibiti utoro wa waalimu mashuleni  ambapo na asilimi 37 wapo shuleni  lakii hawapo darasani kufundisha “ Amesema Nzunda

Amewataka kujenga mahusiano mazuri kwenye maeneo ya shule  kwa kuwa taaluma haiwezi kufanikiwa  mahali ambapo hakuna utendaji kazi wa pamoja na waone waajiri wanawadhamii na shule kunakuwa ni mahali  pazuri pa kuishi na kufanyia kazi.

Aidha amewaonya Makatibu Tawala na Wakurugenzi kutokufanya maamuzi ya mihemko katika suala zima la kuwaonya waalimu bila kufanya utafiti wa kina kuhusu chanzo cha tatizo la kushindwa  kufaulisha vizuri mashuleni kwao kwa kuwa ni watumishi wa umma, hivyo waheshimiwe  wadhaminiwe  kulingana na taluma yao na wafuate she ria na taratibu za utumishi wa umma.

Badhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Elimu, Ofisi ya RAIS, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OT-TAMISEMI), Tixson Nzuda (hayupo pichani) kwenye kikao kazi cha kujadili muelekeo wa masuala mbalimbali ya maendeleo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Elimu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Tixson Nzuda akiwa na Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dkt.Dorothy Gwajima wakiwa katika kikao kazi cha kujadili muelekeo wa masuala mbalimbali ya maendeleo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *