Habari za Wizara

Takwimu sahihi za watu wenye ualbino zitasaidia utoaji wa huduma bora

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akizikiliza jambo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa walemavu wa ualbino wakati wa maadhimisho ya 13 ya Kitaifa na ya 4 Kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Simiyu.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Josephat Sinkamba Kandege  amesema  kuwepo kwa takwimu sahihi  kutawezesha  utoaji wa huduma muhimu  za madawa na kinga ya mionzi  ya jua kwa watu wenye albino ambacho ndicho chanzo kikubwa  cha matatizo ya kansa ya ngozi.

Akihutubia wananchi katika maadhimisho  ya siku ya Kitaifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yaliyofanyika leo Mkoani Simiyu Mhe. Josephat Sinkamba Kandege amesema  amesema takwimu sahihi itasaidia  kupanga mipango mbalimbali ya kuwasaidia watu wenye Albino hasa katika changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jamii.

Amesema kuwa Serikali kupitia Idara ya Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeweka utaratibu wa kufuatilia sensa ya watu wenye albino ambapo kupitia Halmashauri zote nchini Idara ya Ustawi wa Jamii imeendelea kufuatilia takwimu sahihi za  watu wenye albino ili kubaini idadi kamili watu wenye albino.

Amesema kuwa takwimu hizo pia zitawezesha kuboresha utoaji wa huduma  za miwani  ili kukabili tatizo la uoni hafifu kwa watu wenye ualbino na kuhakikisha uimarishaji mipango na bajeti katika  Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Amesema kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango imeanzisha Cost Center ya Ustawi wa Jamii kwenye MTEF  za Halmashauri ambapo ndipo mahala shughuli za bajeti kwa watu wenye ualbino hii itasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji  kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe. Kandege amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa waraka wa utekelezaji wa watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 ikiwemo uanzishwaji wa Kamati za watu wenye ulemavu ambapo kamati hizi zinatoa fursa ya watu wenye ulemavu wakiwemo wenye ualbino kujadilisha na kuzipatia majibu changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Mhe. Kandege amesema kuwa Serikali itaendelea kuteua na kuwezesha watu wenye ualbino kuwa katika sehemu mbalimbali za maamuzi na za kiutendaji ili jamii iweze kuondoa tofauti na kutoa hadhi sawa na watu wenye ualbino.

Aidha ametoa rai kwa Makatibu Tawala Mikoa kuhakikisha  wanakamilisha uundaji wa kamati  za watu wenye ulemavu kuanzia  ngazi za Mikoa, Wilaya Kata na Kijiji ili kuwa na uwazi katika kutoa maamuzi ya watu wenye ualbino.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akiongea na baadhi ya watu wenye ulemavu wa ualbino wakati wa maadhimisho ya 13 ya Kitaifa na ya 4 Kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Simiyu.
 Baadhi wa watu wenye ulemavu wa Ualbino wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya 13 ya Kitaifa na ya 4 Kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yaliyofanyika leo katika Mkoa wa Simiyu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *